Latest News


More

KIJANA TUNZA WOKOVU WAKO

Posted by : Unknown on : Wednesday, June 4, 2014 0 comments
Unknown
Saved under : ,
Nataka niongee na vijana wanaosema wameokoka, wa kike kwa wa kiume. Unakiri umeokoka, unatumika nyumbani mwa Bwana kanisani na kwenye huduma mbalimbali. Unaongoza sifa, unaimba sifa, anapiga vyombo, unahubiri, shemasi na mengine mengi na unategemewa hasa katika mwili wa Kristo. Ila sasa pale unapopata mchumba au unapoona kuwa umepata mchumba unasahau kabisa kuwa wewe ni mtumishi wa Mungu, umezibeba chapa ya Yesu, chumvi ya ulimwengu.
Yani vijana wa siku hizi wakishaambiana nakupenda nitakuoa wanaona tayari wameshaoana. Ile tabia ya watoto wa Mungu inapotea kabisa ndani yao, wanaanza kuishi sawa na watu wasiomjua Mungu. Bado hamjafunga ndoa ila kila siku upo nyumbani kwa kaka huyo anapika, unafua na kufanya usafi, hamjaoana ila mkiwa peke yenu mnashikana shikana, kupigana mabusu na kuamshana hisia kabla ya wakati wake.
Kila saa mnachat habari za sex, na mambo yanayofanana na hayo, hadi kutumiana picha zisizofaa. Upo wapi wokovu wako? Kwanini umkosee Mungu kwa jambo ambalo unaweza kusubiri wakati wake ufike? Hivi baada ya kuchat hivyo mnavyochat baada ya kutenda hayo mnayotenda, unapata ujasiri wa kusimama mbele za Mungu??
Mungu awasaidie sana vijana wa kizazi cha sasa

No comments:

Leave a Reply