Latest News


More

NJIA YA KWENDA UZIMANI

Posted by : Unknown on : Wednesday, July 2, 2014 0 comments
Unknown


JAMBO LA KWANZA
Ni kweli kabisa Biblia imeandika kuwa “waitwao ni wengi bali wateule ni wachache”.Lakini pia haikukosea kabisa kuandika na kusomeka kana kwamba kwenye maji,kila aonaye na aone kwa wepesi kuwa “Si kila mtu aniitaye Bwana atakayeingia Mbinguni”,na kama ni hivyo basi,je ni akina nani watakaoingia Mbinguni?.Ni dhahiri kabisa ni wale tu walioandikwa majina yao kwenye kitabu cha UZIMA wa Milele cha Mwanakondoo.
JAMBO LA PILI
Ni ukweli usiopingika kuwa watu wote walioamini kwa mioyo yao na kukiri kwa vinywa vyao kuwa Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi,hakika hao WAMEOKOKA.(Warumi 10:9-10).
   Lakini kwa habari ya UTUMISHI WAKO NDANI YA YESU ni tofauti kabisa.Tuelewe VITU HIVI VIWILI.
1)Watu wote waliokoka wanamtumikia Mungu.
2)Lakini Si wote waliokoka wanalitumikia KUSUDI LA MUNGU.
KWAHIYO NI VYEMA KILA MTU AKATAMBUA kusudi LILILOPO NDANI YAKE KISHA AKAMDHIHIRISHA MUNGU KWA HILO.

No comments:

Leave a Reply