Latest News


More

MAVAZI YASIYOFAA KWENYE NYUMBA ZA IBADA

Posted by : Unknown on : Sunday, July 6, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :
Imekua jambo la kawaida miaka ya hivi karibuni kukuta waumini wa dini ya Kikristo wakiingia kwenye nyumba za ibada na mavazi yasiyompa Mungu utukufu
Mara nyingi unaweza kuwaona wakina dada wakiwa wamevaa mavazi yanayoacha sehemu kubwa ya miili yao nje.Na si wanawake tu hata wanaume nao wameingia kwenye mkumbu huo wa kuvaa nguo za ajabu
Baadhi ya makanisa yamefikia mahali pa kuweka sheria na taratibu kwamba huwezi kuingia kwenye makanisa yao kama haujavaa mavazi yanayompa Mungu utukufu, na kama utafanya hivyo basi unatolewa nje na huruhusiwi kuabudu

Jana nilipata nafasi ya kuabudu katika kanisa la Roman Catholic la St.Peter Oysterbay na kukuta wameweka utaratibu mzuri na bango kubwa getini (kama linavyoonekana hapo juu) la kuonyesha mavazi ambayo hayaruhusiwi kuvaliwa kanisani hapo

Huu ni utaratibu ambao nadhani ni mzuri hata kuigwa na makanisa mengine ili nyumba ya Mungu iheshimiwe na watu wote wanaoingia kusali na muumini mmoja au wachache wasifanye wengine kukosa uchaji kwenye kanisa

No comments:

Leave a Reply