Viungo vya binadamu vikiwa vimefungwa mafurushi
Viungo mbali mbali vya binadamu vimekutwa katika eneo la kutupa taka la Bunju mjini Dar es Salaam katika mazingira ambayo haijafahamika mara moja kuwa viungo hivyo vimetoka wapi.
Kwa mjibu wa Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema viungo hivyo vya binadamu vilivyokutwa ni miguu,vidole ambavyo vilikutwa vikiwa vimefungwa ndani ya mifuko.
Hata pamoja na viungo hivyo pia vifaa vya upasuaji vimekutwa zikiwemo glovuzi.
Mtu mmoja anashikiliwa kuhusishwa na tukio hilo ambaye ni dereva aliyekuwa akiendesha gari hilo lililobeba viungo hivyo vya binadamu.
Haijafahamika mara moja miili hiyo ya binadamu imetolewa wapi na ilipelekwa eneo hilo kwa lengo gani.
Katika miaka ya hivi karibuni Tanzania imekuwa ikikabiliwa na tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino ambapo viungo vyao huchukuliwa,japo kuwa viungo hivi vilivyokutwa kwa sasa bado havihusishwi moja kwa moja na matukio ya mashambulizi na mauaji ya walemavu hao.
(Source: BBC Swahili)
No comments: