Leo jumapili katika Usharika wa Mwenge wa Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania umefanyika mkutano mkuu wa Usharika.Mkutano huo ambao
umeongozwa na mwenyekiti ambaye pia ni mchungaji kiongozi wa Usharika huo
mchungaji Kaanasia Msangi pampja na wazee wa kanisa wanaomaliza muda wao chini
ya katibu msaidizi mzee Ester Palangyo
Mkutano huo ambao umetanguliwa na ibada ya jumapili ambayo
pia ilikua na tendo la kuwaingiza kazini
wazee wapya waliochaguliwa kuongoza usharika huo kwa kipindi cha miaka mine ijayo
Pamoja na mambo mengine mkutano huo ulipokea taarifa ya
mapato na matumizi ya kipindi cha mwaka 2013 na kazi ya ujenzi wa kanisa
inayoendelea kanisani hapo
Pichani juu mchungaji kiongozi Kaanasia Msangi ambaye pia
alikua mwenyekiti wa kikao hicho akiongoza mkutano huo mkuu wa Usharika
No comments: