Wanaume wanaokwepa kutahiriwa wajikuta taabani kwa kufanyiwa kitendo hicho kwa lazima Kenya
Nchini Kenya ambapo wanaume kutoka kabila la Turkana na
makabila mengine ambayo hayana utamaduni wa kutahiri wanaume sasa wanaishi kwa
hofu baada ya baadhi yao kutahiriwa kwa lazima.
Vijana kutoka kabila la Bukusu wamekuwa wakiwavamia wanaume ambao
hawajatahiriwa katika mji wa Moi's Bridge na kuwapaka matope na maji taka na
kisha kuwatahiri hadharani kando ya barabara .Wabukusu huchukulia mtu asiyetahiriwa kuwa mchafu na mwoga, lakini wanaume wanaotahiriwa bila ridhaa yao wanalalamika kuwa wanatwikwa utamaduni usio wao.
Odeo Sirari ambaye yupo katika mji huo wa Moi's Bridge amekutana na vijana hao na kutuandalia taarifa ifuatayo.
No comments: