Latest News


More

JUMUIYA YA SAREPTA (USHARIKA WA BOKO K.K.K.T ) WAMUAGA MZEE MSTAAFU MAMA CECILIA URIO

Posted by : Unknown on : Monday, February 2, 2015 0 comments
Unknown
 Jumuiya ya Sarepta ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Usharika wa Boko jumamosi iliyopita ilifanya ibada ambayo ilikua ni maaluma ya kumwaga mzee wa Kanisa wa jumuiya hiyo aliyestaafu
Katika ibada jiyo iliyoongozwa na Mwinjilisti wa Usharika wa Boko Joyce Mshahara ikiwa na kichwa cha somo kisemacho "UTUKUFU WA BWANA UNATUNG'AZIA) na kuhudhuriwa na wanajumuiya wengi wa jumuiya hiyo ilifanyika nyumbani kwa mzee wa kanisa wa jumuiya hiyo mama Makweta

Pichani mratibu wa jumuiya jiyo akiwa amekaa na mwinjilisti Joyce Mshahara wakati wa ibada hiyo

 Mwenyekiti wa jumuiya ya Sarepta akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi .
 Msoma risala akisoma risala kabla ya utoaji wa zawadi . Akisoma risala hiyo alisema jumuiya hii ilianzishwa miaka minne iliyopita ikiwa na wanajumuiya 30
Mwaka 2012 ililazimika kugawa jumuiya hii kutokana na kuwa na wingi wa wakristo na kuzaliwa jumuiya tatu yaani jumuiya ya Boko Beach, jumuiya ya Jordan na jumuiya ya Sarepta
Mpaka sasa jumuiya hii ina wanajumuiya 84 waliojiandikisha
Mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzisha jumuiya hii ni pamoja na kubariki ndoa 6 kwa pamoja na ndoa nyingine 6 za familia moja moja ambapo zilifanyika mwaka 2014
Lengo kwa mwaka huu ni kufanya kazi ya kuwarejesha walio nje ya kundi kumrudia bwana
 Picha ya pamoja ya wanajumuiya pamoja na viongozi wa jumuiya ya Sarepta na mchungaji kiongozi wa Usharika wa  Boko Mchungaji Mwakyusa (aliyevaa kola)


 Mama Cecilia Urio (mzee wa kanisa mstaafu) akiongea mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake kwenye ibada hiyo
 Kutoka kushoto mzee wa kanisa Anael Isangya, Mzee mama Makweta, Cecilia Urio (mzee wa kanisa mstaafu), Mchungaji Mwakyusa na mwinjilisti Joyce Mshahara
 Mzee Anael Isanya akimkabidhi mchungaji Mwakyusa zawadi yake aliyopewa na wanajumuiya ya Sarepta

 Mwnijilisti Joyce Mshahara naye akipokea zawadi toka kwa mzee wa kanisa mzee Anael Isangya
Mchungaji Mwakyusa akisema neno baada ya kwisha zoezi la utoaji wa zawadi
Waliopewa zawadi ni Mzee Cecilia Urio (aliyestaafu), mzee Isangya na Mama Makweta (wazee wakanisa wapya), mchungaji Mwakyusa na Joyce Mshahara mwinjilisti wa Usharika wa Boko

No comments:

Leave a Reply