Mtoto wa miaka 12 ameshtakiwa kwa
jaribio la kumuua mamake kwa kumpokonya iphone
Mtoto wa miaka 12
amewashtua wengi baada ya kujaribu kumuua mamake mara mbili kwa sababu
alimpokonya simu yake ya Iphone.
Kulingana na afisa
anayesimamia usalama katika jimbo la Colorado Marekani mtoto huyo alimtilia
sumu mamake kwa nia ya kulipiza kisasi.
Mamake aliripotiwa
kuzidiwa hali Machi tarehe mbili baada ya kubugia mchanganyiko wa maziwa na
barafu''smoothie'' lakini ikabainika kuwa mchanganyiko huo ulikuwa
umetayarishwa kwa aina ya sabuni majimaji.
Mamake aliwaambia
maafisa wa polisi kuwa alipigwa na bubumbuazi aliponusia harufu ya sabuni baada
ya kunywa mchanganyiko huo uliotayarishwa na mwanawe.
''mara ya kwanza
nilidhania kuwa hakusuza vizuri glasi aliyoniandalia nayo lakini baada ya hapo
akapata sabuni hiyohiyo katika buli lake la maji ndipo akagutuka''alisema mama
huyo
Mwanawe alimwambia kuwa
alikuwa ameudhika sana na haua yake ya kumpokonya Iphone na kuwa alikuwa
amefanya jaribio mbili ya kumtoa uhai.
Mamake alikimbizwa
hospitali iliyokaribu ya mji wa Boulder kabla ya kuwaita maafisa wa polisi na
kutoa ripoti hiyo.
Uchunguzi uliofwatia
ukiongozwa na na sajini Bill Crist ulibaini nia ya mtuhumiwa kwa mjibu wa
jarida la BuzzFeed .
Mtoto huyo alikamatwa
tarehe 20 Machi na kufikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya watoto
alikoshtakiwa kwa jaribio la kumtoa uhai mamake .
“amejaribu mara kadha
kumtoa uhai mamake '' alisema sajini Crist.
Mamake kwa sasa
ameruhusiwa kurejea nyumbani lakini bila shaka akiwa mwangalifu zaidi.
Idara ya haki katika
jimbo hilo inaendelea na uchunguzi.
No comments: