Mtoto muathirika wa utesaji nyumbani
Picha ya kushtusha
imeachiliwa kwa ulimwengu hivi karibuni picha inayomuonesha mtoto mdogo mwenye
umri wa miaka mitano aliye kondeana ,aliyetelekezwa katika sehemu ya chini ya
nyumba yao ,aliyefungiwa na kuachwa afe njaa na familia yake.
Tammi Bleimeyer,mwenye
umri wa miaka 33,na mumewe Bradley,mwenye miaka 24, wameshtakiwa kwa kosa la
kuhatarisha uhai wa mtoto wao baada ya kumkuta mtoto huyo akiwa katika hali
dhoofu katika majira ya baridi ,kitongoji cha Harris, huko Texas.
Askari aliye fanikisha
kupatikana kwa mtoto huyo Mark Herman,amesema kwamba amefanya kazi ya polisi
katika kipindi cha miaka thelathini lakini hajawahi kushuhudia tukio lanamna
hii.
Askari huyo anasema
wamemkuta mtoto huyo katika hali mbaya ana njaa kali,amekondeana,amevilia damu
mwilini kama aliyekuwa akipigwa ama kupitia mateso makali na ngozi yake
ilionekana kama imeachana na mifupa ,ilikuwa ni hali ya kutisha sana kumwona
mtoto katika hali hiyo.
Bradley alikuwa
akibishana na mtoto huyo wa kambo mwenye umri wa miaka kumi na sita aliyekuwa
akiwataka wazazi wa mtoto huyo kuacha kumfungia mtoto wako katika chumba cha
chini ya ardhini nyumbani mwao .
Na polisi walipofika
nyumbani hapo waligundua chumba kidogoo,chini ya nyumba hiyo kikiwa kimefungwa
na godoro tu ndani yake na mtoto aliyeketi juu ya godoro ,ingawa mama wa kambo
wa mtoto huyo alimtorosha baada ya kujua kwamba polisi wanamfuatilia, na
kumkuta katika chumba cha hoteli na kumfuatilia hatimaye kumchukua mtoto huyo
na kumpeleka hospitalini kwa matibabu.
Ingawa mpaka mtoto huyo
anafikishwa hospitalini, sababu za kufungiwa kwa mtoto huyo hazikufahamika mara
moja ,na wazazi wa mtoto huyo wamekataa kuzungumzia tukio hilo .
Baba wa mtoto huyo
anashikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo, na mtoto wake bado amesalia
hospitalini kwa matibabu zaidi katika hospitali ya watoto iliyoko mjini Texas .
(Source:BBC Swahili)
No comments: