Written by Anonymous

HAPPY NEW YEAR 2015

by Anonymous / 06 Jan 2015

...

Written by Anonymous

MERY CHRISTMAS

by Anonymous / 25 Dec 2014

WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRIS...

Written by Anonymous

HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUZINDUA ALBUM YAO MWEZI APRIL

by Anonymous / 31 Mar 2014

 Kikundi cha Hamugembe Praise and Worship Team cha mjini Bukoba  kinatarajia kuzindua album yao ya nyimbo za kusifu na kuabudu ...

Written by Anonymous

WE WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2014

by Anonymous / 31 Dec 2013

Leo ndio siku ya mwisho kwa mwaka huu 2013 na masaa machache yajayo tutaingia mwaka ujao 2014.Mtandao huu unawatakia kila la kheri na ba...

Written by Anonymous

KWAYA KUU YA USHARIKA WA AZANIA FRONT NDIO MABINGWA WA UIMBAJI WA K.K.K.T – DMP

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Written by Anonymous

MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH LEO

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

KUTOKA MADHABAHUNI

IBADA KATIKA KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE JUMAPILI HII

Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi  (pichani juu) aliongoza na kuhubiri Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa m...

More KUTOKA MADHABAHUNI
More NENO LA LEO
More MAHUBIRI
More MAOMBI

HABARI ZA KIDINI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MHESHIMIWA MAKONDA AZINDUA VITABU VYA INJILI KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE KAWE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe Bwana Makonda (pichani juu) alimsh...

More HABARI ZA KIDINI

More HABARI ZA KIDINI

JINSI YA KUSHINDA KINYONGO

Posted by : Unknown on : Tuesday, April 21, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :

Mke aliyemwekea kinyongo mume wake

KIKWAZO

Unashindwa kusahau mambo mabaya ambayo mwenzi wako alisema au kutenda; maneno yake makali na matendo ya kutojali yamebaki akilini mwako. Hivyo, badala ya kuwa na upendo umekuwa na kinyongo. Inaonekana kwamba huwezi kufanya lolote ila tu kuvumilia ndoa isiyo na furaha. Hilo pia linafanya uwe na kinyongo na mwenzi wako.
Uwe na hakika kwamba unaweza kurekebisha hali hii. Hata hivyo, kwanza chunguza mambo machache kuhusu kinyongo.

UNACHOPASWA KUJUA

Mume na mke wakiwa kwenye baiskeli iliyozuiwa na nanga
Kuweka kingyongo husababisha kikwazo kinachozuia ndoa yako kusonga mbele
Kinyongo kinaweza kuharibu ndoa. Kwa nini? Kwa sababu kinadhoofisha sifa ambazo ni msingi wa ndoa, kama vile upendo, uaminifu, na ushikamanifu. Hivyo basi, kinyongo si kisababishi cha matatizo ya ndoa, bali kinyongo ni tatizo la ndoa. Kwa kufaa Biblia hutushauri tuondolee mbali “uchungu wote wenye uovu.”—Waefeso 4:31.
Ukiwa na kinyongo, unajiumiza mwenyewe. Kuweka kinyongo ni kama kujipiga kofi na kutarajia mtu mwingine ahisi uchungu. “Huenda mshiriki wa familia ambaye una kinyongo naye anahisi vizuri, anafurahia maisha, na labda hasumbuliwi na hali hiyo,” akaandika Mark Sichel katika kitabu chake Healing From Family Rifts. Somo ni nini? “Kinyongo kinakuumiza kuliko kinavyomuumiza mtu uliyemwekea kinyongo,” anasema Sichel.
Kuweka kinyongo ni kama kujipiga kofi na kutarajia mtu mwingine ahisi uchungu
Wewe ndiye unayeamua kuwa na kinyongo. Watu fulani hawaamini hivyo. Wanasema, ‘Mwenzi wangu ndiye aliyefanya niwe na kinyongo.’ Tatizo ni kwamba mawazo kama hayo yanakazia jambo ambalo haliwezi kudhibitiwa, yaani, matendo ya mtu mwingine. Biblia inatoa suluhisho. Inasema hivi: “Kila mmoja na athibitishe kazi yake mwenyewe.” (Wagalatia 6:4) Hatuwezi kudhibiti maneno au matendo ya mtu mwingine, lakini tunaweza kuamua jinsi tutakavyotenda. Kuweka kinyongo si suluhisho.

 UNACHOWEZA KUFANYA

Chukua hatua. Ni rahisi kumlaumu mwenzi wako. Lakini kumbuka, wewe ndiye unayeamua kuwa na kinyongo. Ndivyo ilivyo pia na kusamehe. Unaweza kufuata himizo hili la Biblia: “Jua lisitue [u]kiwa katika hali ya kuchokozeka.” (Waefeso 4:26) Ukiwa tayari kusamehe utafanikiwa kutatua matatizo yako ya ndoa kwa njia ya utulivu.—Kanuni ya Biblia: Wakolosai 3:13.
Jichunguze kwa unyoofu. Biblia inasema kuna watu wenye “hasira” na wenye “mwelekeo wa ghadhabu.” (Methali 29:22) Je, wewe uko hivyo? Jiulize hivi: ‘Je, nina uchungu moyoni? Je, mimi hukasirika haraka? Je, mimi hukasirishwa na mambo madogo-madogo?’ Biblia inasema kwamba “anayeendelea kuongea juu ya jambo anawatenganisha watu wanaofahamiana.” (Methali 17:9; Mhubiri 7:9) Hilo linaweza pia kutokea katika ndoa. Basi, kama una mwelekeo wa kuweka kinyongo, jiulize, ‘Je, ninaweza kuwa mwenye subira zaidi kumwelekea mwenzi wangu?’—Kanuni ya Biblia: 1 Petro 4:8.
Amua jambo muhimu zaidi. Biblia inasema kuna “wakati wa kukaa kimya na wakati wa kusema.” (Mhubiri 3:7) Si lazima uzungumzie kila kosa; wakati mwingine unaweza ‘kusema moyoni mwako, ukiwa kitandani mwako, na kunyamaza.’ (Zaburi 4:4) Unapohitaji kuzungumzia tatizo fulani, subiri mpaka hasira yako ishuke. Mke anayeitwa Beatriz anasema: “Ninapokasirika, mimi hujitahidi kutulia kwanza. Hatimaye, mimi huona kwamba halikuwa tatizo kubwa, na inakuwa rahisi kwangu kuzungumza kwa heshima.”—Kanuni ya Biblia: Methali 19:11.
Elewa maana ya “kusamehe.” Katika Biblia, wakati mwingine neno “kusamehe” hutafsiriwa kutokana na neno la awali linalomaanisha kuachilia kitu fulani. Kwa hiyo, kusamehe hakumaanishi kupuuza kosa kana kwamba halikutokea; kunamaanisha kuachilia kosa. Kwa sababu unatambua kwamba kuweka kinyongo kunaweza kukudhuru kiafya na kuvuruga ndoa yako hata kuliko kosa lenyewe.
Saved under :

No comments:

Leave a Reply