Written by Anonymous

HAPPY NEW YEAR 2015

by Anonymous / 06 Jan 2015

...

Written by Anonymous

MERY CHRISTMAS

by Anonymous / 25 Dec 2014

WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRIS...

Written by Anonymous

HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUZINDUA ALBUM YAO MWEZI APRIL

by Anonymous / 31 Mar 2014

 Kikundi cha Hamugembe Praise and Worship Team cha mjini Bukoba  kinatarajia kuzindua album yao ya nyimbo za kusifu na kuabudu ...

Written by Anonymous

WE WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2014

by Anonymous / 31 Dec 2013

Leo ndio siku ya mwisho kwa mwaka huu 2013 na masaa machache yajayo tutaingia mwaka ujao 2014.Mtandao huu unawatakia kila la kheri na ba...

Written by Anonymous

KWAYA KUU YA USHARIKA WA AZANIA FRONT NDIO MABINGWA WA UIMBAJI WA K.K.K.T – DMP

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Written by Anonymous

MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH LEO

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

KUTOKA MADHABAHUNI

IBADA KATIKA KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE JUMAPILI HII

Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi  (pichani juu) aliongoza na kuhubiri Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa m...

More KUTOKA MADHABAHUNI
More NENO LA LEO
More MAHUBIRI
More MAOMBI

HABARI ZA KIDINI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MHESHIMIWA MAKONDA AZINDUA VITABU VYA INJILI KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE KAWE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe Bwana Makonda (pichani juu) alimsh...

More HABARI ZA KIDINI

More HABARI ZA KIDINI

WATOTO: KWA NINI DAUDI HAKUMWOGOPA GOLIATH

Posted by : Unknown on : Tuesday, April 21, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :


Daudi


Daudi—Kwa Nini Hakuogopa

JE, UMEWAHI kuogopa?— * Wengi wetu tunaogopa mara kwa mara. Unaweza kufanya nini unapoogopa?— Unaweza kumwomba msaada mtu mkubwa na mwenye nguvu kuliko wewe. Labda baba au mama yako anaweza kukusaidia. Tunaweza kujifunza mengi kutoka kwa Daudi kuhusu mahali tunapoweza kupata msaada. Alimwimbia Mungu hivi: “Mimi nitakutegemea wewe. . . . Nimeliweka tegemeo langu kwa Mungu; sitaogopa.”—Zaburi 56:3, 4.
Unafikiri Daudi alijifunza kutokuwa mwoga kutoka kwa nani? Kutoka kwa wazazi wake?— Bila shaka alijifunza hilo kutoka kwao. Baba yake, Yese, alikuwa mzee mwaminifu wa ukoo wa Yesu Kristo, “Mkuu wa Amani” aliyeahidiwa wa Mungu. (Isaya 9:6; 11:1-3, 10) Baba ya Yese, yaani, babu ya Daudi, alikuwa Obedi. Kitabu kimoja cha Biblia kina jina la mama ya Obedi. Je, unajua jina lake?— Ni Ruthu, mwanamke mshikamanifu aliyekuwa mke wa Boazi.—Ruthu 4:21, 22.
Bila shaka, Ruthu na Boazi walikufa muda mrefu kabla ya Daudi kuzaliwa. Huenda unajua jina la mama ya Boazi, yaani, nyanya ya nyanya ya Daudi. Aliishi Yeriko na alisaidia kuwaokoa wapelelezi fulani Waisraeli. Kuta za Yeriko zilipoanguka, alilindwa pamoja na familia yake kwa kuning’iniza kamba nyekundu katika dirisha lake. Jina lake ni nani?— Ni Rahabu ambaye alikuja kuwa mwabudu wa Yehova, na ni mfano wa ujasiri unaopaswa kuigwa na Wakristo.—Yoshua 2:1-21; 6:22-25; Waebrania 11:30, 31.
Tunaweza kuwa na hakika kwamba baba na mama ya Daudi walimfundisha kuhusu watumishi hao waaminifu wa Yehova kwa kuwa wazazi waliamriwa wawafundishe watoto wao mambo kama hayo. (Kumbukumbu la Torati 6:4-9) Wakati ulifika ambapo Samweli nabii wa Mungu aliambiwa amchague Daudi, mwana mchanga zaidi wa Yese, kuwa mfalme wa wakati ujao wa Israeli.—1 Samweli 16:4-13.
Siku moja, Yese alimtuma Daudi awapelekee chakula kaka zake watatu waliokuwa wakipigana na adui za Mungu, Wafilisti. Daudi anapofika, anakimbia kwenda kwenye uwanja wa mapigano na anasikia jitu linaloitwa Goliathi likivitukana  “vikosi vya Mungu aliye hai.” Watu wote wanaogopa kupigana na Goliathi. Mfalme Sauli anasikia kwamba Daudi yuko tayari kupigana na jitu hilo, hivyo anamwita. Lakini Sauli anapomwona Daudi, anamwambia: “Wewe ni mvulana tu.”
Daudi anamweleza Sauli kwamba alimwua simba na dubu waliojaribu kuchukua kondoo wa familia yake. Goliathi “atakuwa kama mmoja wa hao,” Daudi anasema. “Nenda, na Yehova awe pamoja nawe,” Sauli anajibu. Daudi anajichagulia mawe matano yaliyo laini kabisa, anayatia katika mfuko wake wa mchungaji, anachukua kombeo lake, na kwenda kupigana na jitu hilo. Goliathi anapomwona mvulana huyo akija, anasema hivi kwa sauti: “Wewe nikaribie tu, nyama yako nitawapa ndege.” Daudi anajibu: “Naja kwako nikiwa na jina la Yehova,” na kisha akasema hivi kwa sauti: “Hakika nitakupiga.”
Daudi akimshinda Goliathi
Baada ya hapo, Daudi anakimbia kumwelekea Goliathi, anachukua jiwe kutoka kwenye mfuko wake, analiweka kwenye kombeo lake, na kulitupa moja kwa moja ndani ya kichwa cha Goliathi. Wafilisti wanapoona kwamba jitu limekufa, wanaogopa na kukimbia. Waisraeli wanawafuatilia na kushinda vita hivyo. Tafadhali soma pamoja na familia yako simulizi hilo lote katika 1 Samweli 17:12-54.
Ukiwa kijana, huenda nyakati fulani ukaogopa kufuata amri za Mungu. Yeremia alikuwa kijana na aliogopa mwanzoni, lakini Mungu alimwambia: “Usiogope . . . kwa maana ‘mimi niko pamoja nawe.’” Yeremia alipata ujasiri na kuhubiri kama Mungu alivyomwagiza afanye. Kama Daudi na Yeremia, ukimtegemea Yehova, wewe pia unaweza kujifunza kuwa jasiri.—Yeremia 1:6-8.

No comments:

Leave a Reply