Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Michezo ya Kompyuta?
Maswali kuhusu michezo ya kompyuta
Nchini Marekani ambako biashara ya michezo ya
kompyuta huingiza mabilioni ya dola . . .
-
Wachezaji wa michezo ya kompyuta wana umri wa miaka mingapi hivi?
-
18
-
30
-
-
Kuna wanaume wangapi wanaocheza michezo ya kompyuta kwa kulinganishwa na wanawake?
-
Asilimia 55 ni wanaume; asilimia 45 ni wanawake
-
Asilimia 15 ni wanaume; asilimia 85 ni wanawake
-
-
Kati ya makundi mawili yafuatayo, ni kikundi gani kilicho na idadi kubwa zaidi ya watu wanaocheza michezo ya kompyuta?
-
Wanawake wenye umri wa miaka 18 na zaidi
-
Wanaume wenye umri wa miaka 17 kwenda chini
-
Majibu (yanategemea habari zilizopatikana mwaka
wa 2013):
-
B. 30.
-
A. Asilimia 45 ni wanawake
—karibu nusu ya wachezaji wote. -
A. Asilimia 31 ya wanawake wenye umri wa miaka 18 na zaidi wanacheza michezo ya kompyuta, ikilinganishwa na asilimia 19 ya wavulana wenye umri wa miaka 17 kwenda chini wanaocheza michezo hiyo.
Takwimu hizo zinaweza kukusaidia kujua tu idadi
ya watu wanaocheza michezo ya kompyuta. Lakini hazikusaidii uone
athari ya kucheza michezo ya kompyuta —iwe ni mazuri au
mabaya.
Matokeo mazuri
Ni maelezo gani kati ya yafuatayo
unayokubaliana nayo kuhusu michezo ya kompyuta?
-
“Ni burudani yenye kuchangamsha inayounganisha familia na marafiki.”
—Irene. -
“Ni njia nzuri ya kusahau matatizo yako.”
—Annette. -
“Inatusaidia kuwa na akili nyepesi ya kufanya mambo.”
—Christopher. -
“Inakusaidia usitawishe ustadi wa kusuluhisha matatizo.”
—Amy. -
“Ubongo wako unazoezwa kufikiri na kupanga mambo pamoja na mikakati mbalimbali.”
—Anthony. -
“Michezo fulani huchochea ushirikiano kati ya marafiki.”
—Thomas. -
“Michezo fulani inakusaidia ufanye mazoezi na kuboresha umbo lako.”
—Jael.
Je, unakubaliana na maelezo yote
yaliyotolewa au ni baadhi tu? Michezo ya kompyuta inaweza
kutunufaisha kimwili na kiakili. Hata ingawa michezo fulani ni ya kupitisha
wakati tu na “ni njia nzuri ya kusahau matatizo yako,” kama Annette alivyosema,
si vibaya kuicheza kwa kusudi hilo.
● Biblia inasema kwamba kuna “wakati wa kila
jambo chini ya mbingu,” kutia ndani tafrija. —Mhubiri
3: 1-4.
Ubaya wake
Je, michezo ya kompyuta inakuibia
wakati?
“Ninapoanza kucheza, inakuwa vigumu sana kuacha. Mimi hujiambia, ‘Acha niendelee kidogo tu!’ Kisha bila kujua, saa kadhaa zinapita na ninajikuta nimecheza kwa muda mrefu sana!”—Annette.
“Michezo ya kompyuta inaweza kukupotezea muda mwingi sana. Unakaa mbele ya kompyuta na kuhisi kwamba umetimiza jambo fulani kwa sababu umeshinda mara tano, lakini ukweli wa mambo ni kwamba hujatimiza jambo lolote.”—Serena.
Jambo kuu: Mtu anapopoteza
pesa, huenda akazipata tena. Lakini sivyo ilivyo unapopoteza wakati.
Kwa njia fulani, wakati una thamani kubwa zaidi hata kuliko pesa. Kwa hiyo
usiruhusu chochote kikuibie wakati wako!
● Biblia inasema: “Endeleeni kutembea kwa
hekima . . . , mkijinunulia wakati unaofaa.” —Wakolosai 4:5.
Je, michezo ya kompyuta imeathiri jinsi
unavyofikiri?
“Matendo ya uhalifu ambayo yanaweza kumfanya mtu afungwe gerezani au ahukumiwe kifo, yanafanywa katika michezo ya kompyuta bila wasiwasi.”—Seth.
“Michezo mingi ya kompyuta inahusisha kuwaangamiza maadui ili mtu apate ushindi. Kwa kawaida, kuna njia kadhaa za kuwaua maadui kwa ukatili.”—Annette.
“Nyakati nyingine huwezi kuamini kile unachowaambia marafiki wako mnapocheza—unawaambia ‘Kufa!’ au ‘Nitakuua wewe!’ ” —Nathan.
Jambo kuu: Epuka michezo
inayotukuza mambo ambayo Mungu anachukia, kutia ndani jeuri, kuwasiliana na
pepo, na ngono haramu. —Wagalatia
5: 19- 21; Waefeso 5: 10; 1 Yohana 2: 15,
16.
● Biblia inaonyesha kwamba Yehova anamchukia
“mtu yeyote anayependa jeuri” —si lazima mtu awe ametenda
kwa jeuri. (Zaburi 11:5) Hata ingawa michezo ya
kompyuta unayochagua haiamui utakuwa mtu wa aina gani, michezo hiyo inaweza
kufunua mambo fulani kukuhusu au jinsi ulivyo.
Fikiria jambo hili: Kulingana na kitabu
kinachoitwa, Getting to Calm, “michezo ya kompyuta yenye jeuri huathiri
sana tabia ya mtu hata kuliko kutazama televisheni, kwa sababu watoto
hawamtazami tu shujaa fulani mkatili anayewaua wengine ovyoovyo, bali wao
wenyewe wanakuwa ndiye shujaa mwenyewe anayetekeleza mauaji hayo. Kwa kuwa
michezo hiyo humfunza mtu kama mwalimu anavyofanya darasani, basi kihalisi mtu
hujifunza kuwa mjeuri anapoicheza.” —Linganisha Isaya 2:4.
Ukweli wa mambo
Vijana wengi wamejifunza kuwa na usawaziko
kuhusiana na kucheza michezo ya kompyuta. Ona mifano hii miwili.
“Nilikuwa nikicheza michezo ya kompyuta hadi usiku sana huku nikijiambia: ‘Hakuna shida, usingizi wa saa tano unanitosha. Acha niendelee kidogo tu.’ Lakini sasa nimejifunza kuwa na usawaziko kuhusiana na kucheza michezo hiyo. Bado ninapenda kuicheza mara kwa mara nipatapo muda. Hata hivyo, kila jambo linapaswa kufanywa kwa kiasi.”—Joseph.
“Kwa kuwa nimepunguza muda niliotumia kucheza michezo ya kompyuta, nimefaulu kutekeleza mambo mengi zaidi! Nimefaulu kuongeza muda ninaotumia katika kazi ya kuhubiri, kuwasaidia wengine kutanikoni, na hata nimejifunza kucheza piano. Kuna mambo mengine mengi ambayo mtu anaweza kufanya kuliko kucheza tu michezo ya kompyuta!”—David.
● Biblia inasema kwamba wanaume na wanawake
wakomavu ni wenye “kiasi katika mazoea.” (1 Timotheo 3: 2, 11) Wao hufurahia burudani, lakini
hawafanyi hivyo kupita kiasi, wanajua wakati wa kuacha kwa kuwa wana sifa ya
kujizuia. —Waefeso 5: 10.
Jambo kuu: Michezo ya
kompyuta inaweza kuwa burudani nzuri ikichezwa na kutengewa wakati unaofaa.
Lakini usiruhusu michezo hiyo ichukue wakati wako na kukufanya ushindwe kukazia
fikira mambo yaliyo muhimu zaidi maishani. Badala ya kukazia fikira jinsi ya
kushinda mchezo fulani wa kompyuta, je, halingekuwa jambo la busara zaidi
kujitahidi kutumia muda na jitihada hizo kufikia miradi yako ili ufaulu katika
maisha halisi?
(Source:www.jw.org)
No comments: