Nifanye Nini Ili Nipate Usingizi wa Kutosha?
Biblia inasema hivi: “
Konzi moja ya pumziko ni afadhali kuliko konzi mbili za kazi ngumu na kufuatilia upepo.” (Mhubiri 4:6) Ikiwa hutalala vizuri, hutatimiza mengi!
-
“Nisipolala vya kutosha, siwezi kufikiri vizuri! Ninashindwa kukazia fikira jambo lolote!”
—Rachel, mwenye umri wa miaka 19. -
“Inapofika saa nane mchana, mimi huwa nimechoka hivi kwamba ninaweza kulala nikiwa ninazungumza na mtu!”—Kristine, mwenye umri wa miaka 19.
Je, unahitaji kulala zaidi? Yafuatayo ni
baadhi ya mambo ambayo vijana wenzako wamefanya.
Epuka kuchelewa kulala.
“
Nimekuwa nikijaribu kulala mapema,” anasema Catherine, mwenye umri wa miaka 18.
Katiza mazungumzo.
“
Wakati mwingine marafiki hunipigia simu au kunitumia ujumbe usiku sana,” anasema Richard, mwenye umri wa miaka 21, “
lakini sasa nimejifunza kukatiza mazungumzo ili nilale.”
Lala na uamke saa zilezile kila siku.
“
Siku hizi mimi hujaribu kulala na kuamka saa zilezile kila siku,” anasema Jennifer, mwenye umri wa miaka 20.
Siri ya Kufanikiwa: Jaribu
kulala kwa angalau saa nane kila siku.
Utapata faida nyingi ukichukua hatua chache
tu ili kupata usingizi wa kutosha. Kumbuka, ukiwa na afya nzuri utakuwa na sura
nzuri, utahisi vizuri, na kutimiza mengi zaidi.
Tofauti na mambo mengine maishani, kuboresha
hali yako ya kimwili ni mojawapo ya mambo ambayo wewe unaweza kufanya.
“
Afya yako,” asema Erin, mwenye umri wa miaka 19, “
inategemea mtu mmoja tu”—wewe.
No comments: