Jambo muhimu la kufahamu ni kwamba agano la kale lilipatiwa taifa la Israeli wala sio wakristo. Baadhi ya sheria hizo zilikuwa za kuwafanya waisraeli wajue jinsi ya kumtii na kumfurahisha Mungu (amri kumi za Mungu kwa mfano), baadhi yazo zilikuwa zikiwafunza jinsi ya kumuabudu Mungu (kwa ile njia ya sadaka), nyengine zilikuwa za kuwafanya waisraeli wawe watu maalum (kama sheria za aina za mavazi na chakula). Hakuna sheria yoyote ya agano la kale inayotumika kwetu sasa. Yesu alipokufa msalabani, alimaliza matumizi ya sheria ya agano la kale (Warumi 10:4; Wagalatia 3:23-25; Waefeso 2:15).
Mahali pa sheria ya agano la kale, tuko chini ya sheria ya kristo (Wagalatia 6:2) ambayo ni, “Mpende bwana Mungu wako na moyo wako wote akili zako zote na nguvu zako zote. Hii ndiyo ya kwanza na amri iliyo kuu. na ya pili ni kama ya kwanza, mpende jirani yako kama nafsi yako. Torati yote na manabii inakamilishwa katika amri hizi mbili” (Mathayo 22:37 – 40). Tukifanya mambo haya mawili tutakuwa tunatimiza yale kristo angetaka tuyafanye, “na huu ndio upendo wa Mungu: kutii amri zake. Na amri zake si nzito” (waraka wa kwanza wa Yohana 5:3). Kwa mtazamo, amri kumi za Mungu hazina uhusiano na wakristo. Hata hivyo, tisa katika amri kumi za Mungu zimerudiwa katika agano jipya (zote isipokuwa ile ya kuweka sabato). Kwa kwaida kama tunampenda Mungu hatutakuwa na miungu miginemila yeye. Tukiwapenda majirani zetu hatutawaua, hatutawadanganya,hatutazini nao, wala kutamani kile walichonacho. Kwa hivyo hatuko chini ya sheria ya agano la kale. Sisi ni wakumpenda Mungu na pia majirani zetu. Tukifanya mambo haya mawili kwa uaminifu wa moyo, kila kitu kitakuwa sawa.
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: