Latest News


More

Posted on : Friday, August 21, 2015 [0] comments Label:

SEMINA YA MTUMISHI WA MUNGU SETH OSCAR - MBEZI MWISHO (MAKABE) KANISA LA EAGT

by : Unknown
"KUTOKA KWENYE VIFUNGO"........ISATA 42:22
Mtumishi wa Mungu Seth Oscar anaendesha mkutano wa  injili katika kanisa la EAGT Mbezi Makabe
Mkutano huo umeanza jumatatu wiki hii na unaenda kuhitimishwa jumapili hii 
Pichani juu mtumishi huyo akihubiri katika mkutano huo wa injili


Pichani juu mtumishi wa Mungu akifungua watu kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya ibilisi

 Watu mbalimbali wakifunguliwa kwenye mkutano huo wa injili

 Uponyaji ukiendelea kwenye mkutano huo






by : Unknown
 Jumapili hii katika kanisa la Living Water Makuti Kawe ilifanyika ibada nzuri na ya baraka tele
Ibada hiyo ambayo pamoja na mambo mengine ilikua na mahafali ya wanafunzi wa Kozi ya Life Transforming iliongozwa na mkuu wa kanisa hilo Apostle Onesmo Ndegi akishirikiana na mwalimu Lilian Ndegi (pichani juu)
 Waumini wakifuatilia ibada hiyo ya jumapili
 Mwalimu Augustino akibubujika kwa maombi katika ibada hiyo
 Apostle Onesmo Ndegi (mkuu wa kanisa la Living Water Center) akifurahi kwenye ibada hiyo.Kushoto kwake ni mwalimu Lilian Ndegi na watenda kazi wengine wa kanisa hilo
 Apostle Ndegi akifurahi kwenye ibada hiyo ya jumapili
 Mchungaji Naomi wa kanisa hilo akiimba kwa furaha

 Pichani juu na chini ni waimbaji wa kwaya ya Living Water Center Makuti Kawe wakiimba kwenye ibada hiyo


 Mpiga drums naye akiwajibika kwa sehemu yake
Waumini wakiimba na kucheza kwenye ibada hiyo ya jumapili

(Picha kwa hisani ya Gospel Kitaa Blog)
Posted on : Wednesday, February 11, 2015 [0] comments Label:

MJUE MWIGIZAJI WA FILAMU YA YESU

by : Unknown





Wakristo wengi wamekua wakifuatilia na kuangalia sinema ambazo zinamhusu Mwokozi Yesu Kristo
Watu wengi wamefanya tafiti mbalimbali na hapa tunawaletea  kuwaletea historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la ''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel,   baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu. KARIBU.
Brian Deacon ndani ya filamu ya ''JESUS''
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo kwenye ndoa hiyo.

Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260 wakijaribishwa kuigiza(screen test)kuona kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.

Brian Deacon miaka iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.

Amesema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani kama yeye(Brian)atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina gani.

watu wakiangalia filamu ya Yesu ambayo bwana Brian Deacon ni mwigizaji mkuu.

Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake kwamba wamsaidie kwani  amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo nasema alikuwa mkristo jina wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka mwanamama huyo.


Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali kurudi kuendelea na kazi.

Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
watumishi wa Mungu wakiwa njiani kwenda kuonyesha filamu ya Yesu katika uinjilisti huko Kongo.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.

(Source://www.gospelkitaa.co.tz
Posted on : Sunday, December 7, 2014 [0] comments Label: ,

IBADA YA FAMILIA - CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI FAMILIA

by : Unknown
 Katika maisha ya siku hizi kuna changamoto nyingi zinazokabili familia mbalimbali
Akihubiri katika ibada ya jumapili ya leo katika Usharika wa Mwengemchungaji Ernest Kadiva wa kanisa la K.K.K.T amesema kuna changamoto nyingi zinazikabili familia zikiwepo;
1.Upendo kupoa pale ambapo na kipato kinapopungua
2.Teknolojia inachangia watoto kuharibika au kutotii mafundisho toka kwa wazazi na kanisa kwa ujumla
3.Familia kukosa nafasi ya kukaa pamoja (baba, mama na watoto) kutokana na mihangaiko ya kutafuta kipato hivyo kuchangia maadili ya watoto kuzidi kumomonyoka
Katika ibada hiyo kulikua na matendo mbalimbali yaliyofanyika kama vile kurudi kundini, ubatizo wa watoto wadodo, kipaimara kwa mkristo mmoja, shukrani za pekee, na ndoa mbili  ambazo zimefungwa hivi leo Usharikani hapo na kisha kujumuika kwa chakula cha pamoja kwa washarika wote
Kwaya na vikundi mbalimbali vilijumuika kuimba ikiwepo kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge , kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza na mwimbaji binafsi mmoja
 Kwaya ya Uinjilisti ya Usharika wa Sinza ikihudumu kwenye ibada hiyo jumapili ya leo
 Waumini wakifuatilia ibada ya leo jumapili katika Usharika wa Mwenge




 Katibu wa baraza la wazee wa Usharika wa Mwenge akifuatilia ibada hiyo.Pembeni ni mzee wa kanisa mama Seka Urio




Posted on : Tuesday, November 11, 2014 [0] comments Label: ,

IWENI WANYENYEKEVU KAMA WATOTO WADOGO - GODWIN GONDWE

by : Unknown
 Yesu Kristo akifundisha wanafunzi wake aliwaambia iweni wanyenyekevu kama walivyo watoto wadogo
Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la .K.K.K.T Usharika  wa mwinjilisti wa kujitegemea Godwin Gondwe alisema watoto wadogo huwa ni wanyenyekevu na hata kama wakiudhiwa huwa ni mara moja tu wanasahau na kufurahi
Bwana Godwin Gondwe ni mtangazaji wa kituo cha habari cha ITV na pia mkufunzi wa chuo kikuu cha Tumaini tawi la Dar es salaam
Ibada hiyo pia ilikua ya kusifu na kuabudu na ilihudhuriwa na vikundi vyote vya kwaya ya Usharika huo kama vile kwaya ya Uinjilisti, Kwaya kuu, kwaya ya Vijana, kwaya ya akina mama na pia mwimbaji wa kujitegemea Mwasabite
Liturjia iliongozwa na mchungaji kiongozi Mchungaji Kaanasia Msangi



 Waumini mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo ya kusifu na kuabudu
 Mwimbaji Mwasabiti akitunzwa na mzee Lema (mzee mstaafu wa kanisa hilo) wakati mwimbaji huyo akiimba wimbo wake wa Ni kwa neema na rehema
 Mwimbaji Mwasabiti akiimba kwa hisani Usharikani Mwenge