Latest News


More

MKUU WA KANISA LA K.K.K.T DR MALASUSA AONGOZA HARAMBEE KUBWA USHARIKA WA MWENGE

Posted by : Unknown on : Thursday, August 8, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :
 Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dr.Alex Malasusa leo ameongoza harambee kubwa ya ujenzi wa kanisa katika Usharika wa Mwenge .Katika ibada hiyo iliyohudhuriwa pia na naibu waziri wa katiba na sheria mheshimiwa Angela Kairuki,  Askofu Dr.Malasusa (pichani juu) aliongozana na viongozi wengine waandamizi wa dayosisi ya Mashariki na Pwani akiwepo msaidizi wa askofu mchungaji Dean Fupe, wakuu wa majimbo ya Dayosisi, wachungaji mbalimbali wa sharika, wawakilishi wa sharika mbalimbali,wageni mbalimbali na wenyeji ambao ni washarika wa Usharika wa Mwenge

Ibada hiyo iliongozwa na mkuu huyo wa kanisa, Msaidizi wa askofu mchungaji Fupe, Mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Anta Muro , mkuu wa jimbo la Magharibi na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi

Mkuu wa Kanisa la K.K.K.T Dr.Malasusa akiongozana na viongozi wengine wa kanisa kuingia ibadani


Akizungumza katika ibada hiyo ya harambee katibu mkuu wa Usharika wa Mwenge mzee Kombe (pichani juu) alisema ujenzi wa kanisahilo ulianza mwaka 2007 na mpaka kanisa hilo kukamilika kabisa linatazamiwa kugharimu kiasi cha shiliingi 1.2 bilioni.na litakuwa na uwezo wa kuchukua waumini 3000 kwa wakati mmoja

Mzee Kombe alisema mpaka sasa ujenzi wa kanisa hilo umekwishafgarimu kiasi cha shilingi 533 milioni.Awamu iliyopo kwa sasa ni awamu ya tano ambayo inatazamiwa kuchukua kiasi cha shilingi milioni 360 ambao utagharimu kuweka granite (sakafu) utengenezaji wa mfumo wa umeme, uwekaji wa milango na madirisha, utengenezaji wa madhabahu, upakaji wa rangi nk

Dada Lulu Mengelea akiwa na mheshimiwa naibu waziti wa katiba na sheria Angela Kairuki.Kulia kwa naibu waziri ni bwana Matemba.Nyuma ni katibu mkuu wa usharika wa Mwenge mzee Kombe

 Washarika mbalimbali wakifuatilia ibada hiyo
 Baadhi ya washarika wakiwa kwenye ibada hiyo
 Kwaya mbalimbali zilihudumu kwenye ibada hiyo.Juu ni kwaya ya Winners ya Ubungo ikiimba kwenye harambee hiyo
 Baadhi ya wajumbe wa kamati ya maandalizi wakijadili jambo nje ya kanisa.Kutoka kushoto ni dada Lulu Mengele Maro, bwana Maro na bwana Silaa

 Kwaya ya Umoja ya Usharika wa Mwenge ikihudumu kwenye ibada hiyo.Kwaya hiyo inaongozwa na mwalimu Kayese





Kwaya mbalimbali zilihudumu kwenye ibada hiyo na mojawapo ni kwaya ya wachungaji na viongozi wakuu
wa Dayosisi akiwepo mkuu wa kanisa Dr Malasusa.Hakika ilikua ni ibada ya aina yake

Pia ilikuwepo kwaya ya wainjilisti na parish workers.Pichani ni parish worker wa Usharika wa Mwenge parish worker Suzan Mwimbe akiongoza kwaya hiyo

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee mzee Davis Chonjo akihojiwa na waandishi wa habari wa Itv na Redio One



Pia ilikuwepo kwaya ya wazee wa kanisa ambao nao walitia fora kwa uimbaji wao


Bwana Matemba (ambae pia alikua Mc wa harambee hiyo) akiongoza kwaya ya wazee wa kanisa
 Wageni mbalimbali wakitambulishwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge (hayupo pichani)

  Mheshimiwa naibu waziri wa Katiba na Sheria, Angela Kairuki katikati akiwa kwenye ibada hiyo.Kushoto kwake ni  bwana Matemba ambaye pia alikua Mc wa harambee hiyo ambaye pia ni mwimbaji wa kwaya ya Winners ya Magomeni.
Kutoka kushoto mkuu wa jimbo  la Kaskazini mchungaji Muro, msaidizi wa askofu mchungaji Fupe na mkuu wa kanisa Dr Alex Malasusa
Wachungaji mbalimbali wakifanya utambulisho kwenye ibada hiyo
Naibu waziri wa Katiba na Sheria mheshimiwa Angela Kairuki akiongea kwenye ibada ya harambee hiyo.Naibu waziri alisisitiza viongozi wa dini kuhubiri na kuombea amanai katika nchi ya Tanzania ili nchi yetu iendelee kuwa kisiwa cha amani
Vitu mbalimbali vilinadiwa kwenye harambee iyo ikiwemo  pikipiki ambayo ilinunuliwa na Rachel Machunde kwa shilingi milioni tatu..Pichani mkuu wa kanisa akimpongeza dada Rachel Machunde kwa kumtolea Mungu sadaka hiyo
Ilikuwepo pia sofa seti (traditional sofa set) ambayo ilinunuliwa bwana Wiliam Ngowi kwa shilingi milioni tatu na laki mbili.Pichani bwana Ngowi akiwana mke wake wakijaribu kukaa kwenye sofa hizo za kitamaduni

Nibu waziri naye alipata nafasi ya kununua saa ya ukutani
Ndugu Kichila (mdau) naye alipata nafasi ya kununua mojawapo ya vitu vilivyoletwa kwenye harambee siku hiyo
Ndugu Assey naye akinunua mojawapo ya vitu vilivyoletwa kwenye harambee hiyo.Pembeni ni mtoto wake bwana Assey
Washarika na wageni mbalimbali wakinunua vitu mbalimbali
Dada Lulu Mengele naye akinunua baadhi ya vitu kwenye harambee hiyo


Kwaya ya Winnera ya Ubungo wakiimba kwenye harambee hiyo
Wazee wa kanisa wakiongoza waumini kutoka kwenye ibada hiyo ya harambee.Kutoka kushoto mzee mama Ngole, mzee mama Chacha na nyuma ni mzee Swai
Wachungaji wakitoka kwenye ibada hiyo
Picha ya pamoja na mkuu wa kanisa 

No comments:

Leave a Reply