Latest News


More

MCHUNGAJI KAANASIA MSANGI AAGWA RASMI USHARIKA WA MBEZI JUU

Posted by : Unknown on : Monday, May 27, 2013 0 comments
Unknown

Mchungaji Kaanasia Msangi jumapili iliyopita aliagwa rasmi toka kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mbezi juu aliokua anatumika kama mchungaji kiongozi wa Usharika huo.Kwa sasa hivi mchungaji Kaanasia Msangi anatumika kwenye usharika wa Mwenge kama mchungaji kiongozi

 Kwaya ya akina mama wa Usharika wa Mbezi juu ikiimba kwenye ibada hiyo

 Mchungaji Kaanasia akiwa na familia yake na baadhi ya wazee waliomsindikiza kwenye ibada hiyo
 Mchungaji Kaanasia akifurahia jambo wakati wa utambulisho huo.Kushoto kwake ni mumewe Bwana Msangi na kulia ni mabinti zake

 Washarika mbalimbali wakimpongeza mchungaji Kaanasia Msangi kwa utumishi wake kwenye Usharika wa Mbezi Juu
 Familia ya mchungaji Kaanasia Msangi ikitambulishwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mbezi Juu
 Mchungaji Kaanasia Msangi akiwa na mumewe Bwana Msangi
 Mchungaji Kaanasia Msangi akiwa kwenye picha ya pamoja na familia yake.Kutoka kushoto Bwana Msangi, Mchungaji Kaanasia na mabinti zake watatu
 Baadhi ya wazee wa kanisa toka Usharika wa Mwenge waliomsindikiza mchungaji wao.Kutoka kushoto Mzee Godlisten Lema (mtumishi), Mzee Uronu na Mzee mama  Ngole

 Picha ya pamoja ya familia ya mchungaji Kaanasioa na baadhi ya wazee wa Usharika wa Mbezi juu na Usharika wa Mwenge.Wa kwanza kulia (aliyevaa miwani)ni Mzee Kawa wa Usharika wa Mwenge
 Picha ya pamoya (familia ya Mchungaji Kaanasia Msangi) na viongozi wa kanisa Usharika wa Mwenge.Kutoka kushoto mstari wa mbele Mzee Lema, Mzee Uronu, Mume wa Mchungaji Kaanasia bwana Msangi, Mchungaji Kaanasia, na mabinti zake .Nyuma aliyevaa kanzu ni mchungai kiongozi wa Usharika wa Mbezi juu.
Mzee Godlisten Lema (mtumishi) na mzee Uronu ambao walimsindikiza mchungaji wao

 
Katika ibada hiyo ambayo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika huo na neno la Mungu kuhubiriwa na mchungaji Kaanasia Msangi
Katika ibada hiyo vikundi mbalimbali viliimba kama kwaya za usharika wa Mbezi juu na kwaya ya Vijana  toka Usharika wa Mwenge waliomsindikiza mchungaji wao

No comments:

Leave a Reply