Latest News


More

USHARIKA WA MWENGE WAPATA PIGO KWA KUFIWA NA MWINJILISTI WAO

Posted by : Unknown on : Monday, August 5, 2013 0 comments
Unknown
 Usharika wa Mwenge wa kanisa la K.K.K.T na jimbo la Kaskazini wamepata pigo kubwa kwa kufiwa na mwinjilisti wao ndugu Charles Ngoma.Mwinjist huyo alifariki kwa ajali ya gari siku ya alhamisi tarehe 01/08/2013 akiwa safarini na watumishi wenzake wakielekea kwenye Bible study huko maeneo ya Maneromango (Kisarawe)
Mwinjilisti huyo alikuwa anatumika katika mtaa wa Kiwangwa katika eneo la missioni huko Bagamoyo mtaa ambao ulikua unatunzwa na Usharika wa Mwenge
Ibada ya kumwaga mwinilisti huyo ilifanyika katika Usharika wa Mwenge na iliongozwa na mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Anta Muro akisaidiana na mchungaji wa Usharika wa Msasani, na mkuu wa jimbo la kusini.Mwinjilisti huyo anatarajiwa kuzikwa leo huko kwao Tanga
Wanakwaya wa kwaya kuu ya Usharika wa Mwenge wakiimba kwenye ibada hiyo ya mazishi

Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo

Baadhi ya wainjilisti wa jimbo la Kaskazini wakiwa kwenye ibada hiyo

Sehemu ya wachungaji wa jimbo la Kaskazini wakiwa kwenye ibada ya kumwaga mtumishi mwenzao









Mwenyekiti wa umoja wa makanisa ya mwenge akitoa rambirambi zao.Umoja huu unajumuisha makanisa ya Moravian, Roman Catholic, Anglikan na K.K.K.T.Pembeni yake ni mkuu wa jimbo la Kaskazini mchungaji Muro

 Wachungaji wa baadhi ya sharika za jimbo la Kaskazini wakiwa kwenye ibada hiyo
 Mke wa marehemu Charles wapili kutoka kulia akiwa kwenye ibada hiyo ya mazishi.Pembeni ni mzee Kombe ambaye ni katibu wa Usharika wa Mwenge


 Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo ya mazishi hiyo jana
 Mchungaji wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akitoa heshima zake za mwisho kwa uchungu mkubwa.Mchungaji Kaanasia alikua kwenye gari pamoja na marehemu.Yeye na wenzake wawili walipata majeraha madogo tu
 Mke wa marehemu Charles Ngoma akisaidiwa kumwaga mumewe
 Wachungaji wakifanya sala ya mwisho kabla ya kuanza safari ya kuelekea Tanga kwa mazishi
Wainjilisti wenzake wakimsindikiza.Jeneza lake lilibebwa na wainjilisti wa jimbo la Kaskazini

No comments:

Leave a Reply