KUMTOLEA BWANA KAMA FURSA YA KUMTUMIKIA MUNGU
Mwinjilisti wa kujitegemea Godilizen Mushi akihubiri katika ibada ya jumapili usharika wa Mwenge leo alisema kumtolea bwana ni fursa ambayo Mkristo anatakiwa kuitumia kumtumikia Bwana
Mithali 3:9
Mali inaweza kusababisha kumdharau au kumheshimu Mungu wako
Mungu anataka tumheshimu kwa mali zetu
Akinukuu katika biblia mtumishi huyu alisema kuna sikukuu kuu tatu za kumtumikia mungu ambazo ni;
1.Sikukuu ya mavuno
2.Sikukuu ya Pasaka
3.Sikukuu ya kukumbuka kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo
Hizi ni sikukuu kuu tatu ambazo hufanyika mara moja kwa mwaka.Tofauti na sikukuu nyingine ambazo hufanyika zaidi ya mara moja
1Nyakati 29:10-14
Vitu vyote tulivyo navyo vyatoka kwa Mungu.Ukija kwa Mungu huwezi kujiuliza umtoleeje Mungu au umtulee nini Mungu
Mungu ametupa dhamana ya kuvitunza vito vyote tulivyo navyo
Swala la kujiuliza ni je Mungu amekubarikia nini?
Ukishajiuliza ndiyo ujue utamtolea nini Mungu wako
Familia ijifunze jinsi ya kumtolea Mungu;kumtolea Mungu sio fever kwa Mungu, kwani humpi Mungu fever bali unamrudishia Mungu shukrwani
FUNGU LA KUMI
Ukiwa una shilingi 1,000,000 ukamtolea Mungu 10,000, mwezi unaofuata anaweza akakupa shilingi 100,999;kwani ndio kiwango chako cha kumtolea Mungu
Luka 21: 1-4
Ubora wa sadaka hupimwa kwa kile ulichobaki nacho na wala si kile ulichomtolea Mungu
Unavyomtolea Mungu lazima uangalie kile ulichobaki nacho au ulichoacha nyumbani kwako
Kama umebarikiwa sana basi utoe vingi na kama umebarikiwa kidogo vivyo hivyo umtolee Mungu kwa kadri alivyokubariki
Sadaka yako na iwe neema kwako na kwa familia yako na wala si laana alimalizia mwinjilisti Mushi
Ibada hiyo iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika huo mchungaji Kaanasia Msangi
Pia katika ibada hiyo kulikua na ushiriki wa chakula cha Bwana kwa ibada zote tatu
Ibada ya kwanza inaanza saa 12: 00 asubuhi, Ibada ya pili inaanza saa 1:00 asubuhi na ibada ya tatu inaanza saa 4:00 asubuhi.Ibada ya pili nay a tatu zinaambatana na shule ya jumapili
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: