Kura zinahisabiwa katika uchaguzi wa rais wa Madagascar - uchaguzi wa kwanza wa rais tangu Rais Marc Ravalomanana kupinduliwa na Andry Rajoelina mwaka wa 2009.
Upigaji kura ulifanywa Ijumaa.
Wanasiasa hao wawili hawakuruhusiwa kugombea urais tena lakini washirika wao wameania uongozi.
Tume ya uchaguzi ya Madagascar imesema matokeo yataanza kupatikana Jumamosi usiku, lakini baadhi ya watu wanasema matokeo yamekuwa yakitoka taratibu mno.
Tume hiyo imesema inaweza kuchukua juma zima hadi matokeo ya mwisho kutangazwa.
Wagombea wawili wanaoongoza ni wale wanaohusishwa na Rajoelina na Ravalomanana.
Hadi Jumamosi jioni Robinson Jean Louis, mgombea anayeungwa mkono na Ravalomanana alioko uhamishoni, akiongoza kwa kura 26.03%
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: