MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA
LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH
Mashindano ya uimbaji wa kwaua kuu ngazi ya Dayosisi ya Kanisa la
Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Mashariki na Pwani
yamefanyika leo katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge
Katika mashindano hayo ambayo mgeni rasmi alikua mkuu wa
Kanisa la K.K.K.T na askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dr Alex Gerhaz
Malasusa
Katika mashindano hayo yaliyojumuisha kanda zote za Dayosisi
hiyo ambazo ni;
1.Kanda ya Kaskazini ambayo iliwakilishwa na kwaya tatu
2.Kanda ya Kati ambayo iliwakilishwa na kwaya tatu
3.Kanda ya Kusini ambayo iliwakilishwa na kwaya tatu
4.Kanda ya Magharibi ambayo iliwakiliswha na kwaya tatu na
5.Kanda ya Kusini Magharibi ambayo hiyo pekee ndiyo iliwakilishwa na kwaya mbili
Kwaya zilizoshiriki ni;
1.Kwaya kuu ya Usharika wa Kipawa
2.Kwaya kuu ya Usharika wa Azania Front
3.Kwaya kuu ya Usharika wa Kisarawe
4.Kwaya kuu ya Usharika wa Yombo
5.Kwaya kuu ya Usharika wa Kimara
6.Kwaya kuu ya Usharika wa Chanika
7.Kwaya kuu ya Usharika wa Ukonga
8.Kwaya kuu ya Usharika wa Kurasini
9.Kwaya kuu ya Usharika wa Mbezi Beach
10.Kwaya kuu ya Usharika wa Temeke
11.Kwaya kuu ya Usharika wa Magomeni
12.Kwaya kuu ya Usharika wa Mbezi Luis
13.Kwaya kuu ya Usharika wa Neema
14.Kwaya kuu ya Usharika wa Kinondoni
Katika mashindano hayo kila kwaya iliimba jumla ya nyimbo
tatu ambayo wimbo wa kwanza ni wimbo wa siku “NINATAKA KUINGIA”ambao uliimbwa
na kwaya zote Wimbo wa pili ni wimbo wa utamaduni na watatu ni wimbo chaguo la kwaya
No comments: