Mashindano ya uimbaji kwa kwaya kuu za kanisa la K.K.K.T - DMP jimbo la Kaskazini yamefanyika jana jumamosi katika Usharika wa Mbezi Beach.Katika mashindano hayo ambapo kwaya ya Magomeni iliibuka washindi wakifuatiliwa na kwaya ya Usharika wa Kinondoni na washindi wa tatu kwaya kuu ya Usharika wa Mbezi Beach
Akizungumza wakati wa kufanya majumuisho ya alama walizopata wanakwaya hao mchungaji Mwaipopo (pichani juu) ambaye ndiye alikua kamisaa wa majaji wote alisema mwaka huu kwaya zote zimeimba kwa ubora na weledi wa hali ya juu tofauti na miaka ya nyuma kabla ya kusitishwa kwa mashindano hayo
Alisema mwaka huu kila kwaya zimeimba kwa ubora wa hali ya juu na nyimbo chaguo la kwaya zote zimetunga wenyewe kitu ambacho alisisitiza waendelee na ubunifu huo
Awali akimkaribisha kamisaa ili aweze kutoa majumuisho ya alama mwenyekiti wa kamati ya uimbaji wa kwaya kuu kwa jimbo la Kaskazini ndugu Gilbert Mushi (pichani juu) alisema mwaka huu katika ngazi ya kanda kulikuwepo na vituo viwili kimoja kikiwa Usharika wa Mwenge (kilichotoa washindi sita) na kitu cha pili kilikua Usharika wa Kunduchi ambacho kilitoa washindi watano.
Washindi hao ndio waliokutana kutafuta mwakilishi wa jimbo ambaye atakutana na kwaya nyingine 11 za majimbo mengine kumtafuta mshindi wa Dayosisi
Mashindano ya Dayosisi yatafanyika siku ya jumamosi ijayo katika Usharika wa Mbezi Beach
Mkuu wa jimbo la kaskazini mchungaji Muro ambaye pia alikua mgeni rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na kamisaa pamoja na majaji wa mashindano hayo mara baada ya kutangazwa washindi
Columnists
Afya Yako
- All post (163)
- Habari za Kidini (361)
- Kutoka Madhabahuni (193)
- Mahubiri (119)
- Maombi (11)
- Ndoa (88)
- Neno la leo (632)
No comments: