Latest News


More

ASKOFU AWATAKA VIJANA KUACHA NDOTO ZA MAISHA YA MKATO

Posted by : Unknown on : Monday, December 30, 2013 0 comments
Unknown




Dar es Salaam. Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Titus Mdoe amewataka
vijana nchini, kuhakikisha wanapata elimu bora itakayowawezesha kufanikisha ndoto zao kwa njia zisizo za mashaka.
Pia Askofu huyo amewasihi vijana kuhakikisha wanapambana na changamoto za ulimwengu zinazoweza kuwaweka katika mazingira ya kuhatarisha maisha yao.
Askofu Mdoe aliyasema jana katika wa Misa Maalumu ya Vijana iliyofanyika katika Ufukwe wa Mbezi Beach, ambapo vijana walitumia nafasi hiyo kuchangia damu zaidi ya uniti 40 katika Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Mdoe alisema ili kufanikiwa bila kutumia njia ya mkato ni lazima kijana apate elimu dunia na ile ya dini itakayomwezesha kuwa kiongozi bora na asiyeweza kutumia rasilimali za umma vibaya.
“Ukiwa kijana mkristu halafu hupendi elimu ni sawa umeiasi dini yako, hakikisheni mnapata elimu dunia na ile ya Mungu itakayowawezesha kuwajenga na kutokuwa na tamaa ya kupata mafanikio kwa njia za mkato,” alisema Askofu Mdoe
Aliongeza: “Mtu anapata elimu dunia pekee na kutokana na kutokuwa na mafunzo madhubuti ya kiimani, akipata kazi anatumia njia za mkato kujipatia fedha na muda mchache utaona kajenga nyumba, atanunua gari na vitu vingine, acheni tamaa na someni.”
Askofu huyo pia alisema kukata tamaa ya maisha ni mwiko; kijana unapoona umekwama aamke na pambana hadi mwisho na atafanikiwa.

“Unamaliza darasa la saba na unafanya vibaya, usikate tamaa, soma kuanzia ngazi ya cheti, diploma, digrii na mwisho utafanikiwa tu,” alisema. Askofu huyo alisema, kutokana na mabadiliko ya utandawazi hivi sasa vijana wengi wamekuwa wakikabiliwa na changamoto lukuki.

No comments:

Leave a Reply