Latest News


More

NENO LA MUNGU LINA NGUVU

Posted by : Unknown on : Sunday, February 23, 2014 0 comments
Unknown

 Mwinjilisti Mwigune akihubiri katika ibada ya jumapili hii Usharikani Mwenge

NENO LA MUNGU LINA NGUVU

Nabii ni mtu aliye heshimika sana na watu wa wakati wa agano la kale
Akihubiri katika ibada ya jumapili jumapili hii katika Usharika wa Mwenge wa kanisa la K.K.K.T Mwinjilisti Mwigune (pichani juu) alisema wakati wa agano la kale nabii aliheshimiwa na hata watawala kama wafalme kwani waliamini kuwa nabii alitumwa na Mungu na kila alichosema kilikua kinatoka kwa Mungu
Kabla ya kufanya jambo lolote hata kama walitaka kwenda vitani ilikua ni lazima wapate ushauri  toka kwa nabii na walimsikiliza na kumtii

NENO LA LEO
Katika siku za leo manabii wamekua wengi na hata imekua ni vigumu kumjua yupi nabii wa kweli na yupi ni wa uongo.Manabii wengine wamekua hata wakipostosha maandiko ya Mungu, na hata ile nguvu iliyokuwepo kwa manabii wa kale hawanayo manabii wengi wa siku hizi
Biblia inasema kupitia kwa nabii yeremia kuwa nabii ni yue aliyeteuliwa na Mungu na anazungumza na Mungu moja kwa moja

Mungu anamwambia Yeremia kuwa amemchagua yeye; na anamtuma akaseme badala yake
Biblia inasema neon la Mungu lina nguvu, ni kama moto unaochoma
Mungu anamwambia Yeremia nitaweka neon langu juu yako

Tunaishi kwenye nyakati za mwisho ambapo biblia inasema watakuwepo manabii wa uongo hivyo kama wakristo inatupasa kujihadhari na kuwa macho alisisitiza mwinjilisti Mwigune
Kazi ya nabii ilikua ni kuwaelekeza watu kwenda katika njia iliyonyooka na inayompendeza Mungu
Pasipokua na neon ndani yetu ni rahisi kudanganyika na hata kupotoshwa na manabii wa uongo
Neno la Mungu lina nguvu; hata uumbaji wa Mungu aliufanya kwa njia ya neon Yohana 1.1-4

 Waimbaji wa sifa wakihudumu kwenye ibada hiyo ya jumapili

 Wasaharika wakiimba nyimbo za sifa kwenye ibada hiyo ya jumapili




 
Ibada hiyo iliongozwa na waimbaji wa kwaya ya Vijana na kwaya ya Uinjiliti ya Usharika wa Mwenge

No comments:

Leave a Reply