Latest News


More

MAOMBI NI SILAHA

Posted by : Unknown on : Sunday, April 6, 2014 0 comments
Unknown

MAOMBI NI SILAHA

Maombi ni mawasiliano kati ya mwanadamu (mkristo ) na Mungu
Akihubiri katika ibada ya jumapili ya leo katika kanisa la K.K.K.T – Usharika wa Mwenge mtheolojia Peter Lema  (pichani juu) amesema  maombi yamekua ni changamoto kubwa sana kwa wakristo wa leo.Maombi yamesababisha watu kutanga tanga toka sehemu moja kwenda nyingine na hata mafarakano kati ya waumini na waumini.

Tunapoomba tunaamini Mungu ana uwezo wa kutupa kile tuombacho alisema mtheolojia huyo.Watu wengine wanaomba kwa sauti kuu,wengine kwa sauti ndogo nk
Lakini kuomba hakuna kanuni au muundo maalum wa kuomba, waweza kuomba ukiwa umekaa, au umesimama, au unatembea au hata ukiwa umelala na Mungu anasikia
Lakini ni vyema kumheshimu Yule unayemwomba hivyo ni vyema kuwa  wanyenyekevu wakati wa kuomba.


 
Watu waliodumu kwenye maombi kwenye biblia waliombaje?
11)      Mfano Bwana Yesu Kristo mara nyingi aliomba kwa kuanguka kifudi fudi
22)      Paulo yeye alipiga magoti  na ndio aliona no utaratibu mzuri kwa unyenyekevu – Efeso 3:14
33)      Daniel yeye alimbomba Mungu kwa kupiga magoti
Lakini hakuna utaratibu maalum wa kuomba



 
Mahali gani pa kufanyia maombi
Biblia haisemi kama kuna mahali maalum pa kuombea, biblia inasema walipo wawili au watatu kwa jina la Mungu; naye yuko katikati yao.
Unaweza kuomba nyumbani, ofisini, kwenye gar ink, ila mahali tunapoamini kama waumini ni kanisani au hekaluni; japo haitufungi kuomba mahali pengine



 
Sehemu yenye utulivu ni nzuri zaidi kwa ajili ya maombi ila mahali popote pale Mungu anatusikia
Maombi yana changamoto nyingi sana na ndio maana saa nyingine hatupati kile tuombacho sababu ya imani haba au malalamiko kwa Mungu

Tunapenda zaidi kupeleka haja zetu kwa watu wengine mfano mchungaji, mwinjilisti n.k tunasahau kuomba wenyewe , tunataka wao ndio watuombee kitu ambacho si sawasawa
Hata kwa wapendwa wengine wanaringa sababu wana karama ya kiMungu walizopewa mfano ya kuomba , kuimba nk
Kitu ambacho kinaweza sababisha maombi yako yasipokelewe



 
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA MAOMBI

1.Kuepuka dhambi , kwani dhambi inamfarakanisha mwanadamu na Mungu Isaya 59:2

2.Kuomba Roho Mtakatifu atusaidie katika kuomba kwani hatujui jinsi ya kuomba
Yesu Kristo ametupa mamlaka yote kwetu.Na anasema lolote utakaloomba kwa jina lake atakupa
Maombi ni kama mbegu unatia ardhini inahitaji uvumilivu wa kuota na kumea

3.Kumbuka kujitakasa – kuomba toba kabla ya mambo yote ili Mungu apate kusikia sala zetu
Tuwe ni watu wavumilivu wa kungojea kile ambacho tunamwomba Mungu kwani hua anajibu kwa wakati wake.Tusiombe kwa mapenzi yetu ila kwa mapenzi ya Roho mtakatifu alihitimisha mtheolojia Lema
Ibada hiyo ilikua ni maalum ya kusifu na kuabudu ambayo hua inafanyika mara moja kwa mwezi na iliongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge Mchungaji Kaanasia Msangi

No comments:

Leave a Reply