“Bibilia inasema nini kuhusu Mkristo kuingia katika madeni? Ni makosa kukopa au kukopesha pesa?”
Jibu: Maneno ya Paulo kwetu katika Warumi 13:8 tusiwe na deni yeyote bali ile ya upendo ni ukumbusho wa wanguvu wa chukizo la Mungu kwa aina yo yote ile ya deni ambazo hazijalibwa kwa wakati ufaao (ona pia Zarubi 37: 21). Kwa wakati huo huo, Bibilia kabisa haiamrishi kinyume na aina zote za madeni. Bibilia inatuonya kuhusu madeni, na kutia moyo hali ya kutokuwa na madeni, lakini haikatazi madeni. Bibilia iko na maneno makali ya hukumu kwa wakopeshaji ambao wanawatusi wale wameshindwa kuwalipa, lakini haiwahukumu wenye deni.
Watu wengine wanauliza juu ya riba ya mkopo wo wote, lakini mara nyingi katika Bibilia tunaona kwamba riba ya kadri inatarajiwa kupokewa katika pesa ambazo zimekopwa (Methali 28:8; Mathayo 25:27). Katika Israeli ya zamani sheria haikukataa kutoza riba katika viwango vya mkopo-zilizopeanwa kwa maskini (Mambo Ya Walawi 25:35-38). Hii sheria ilikuwa na maana katika maisha ya, kawaida, kifedha, na kiroho, lakini mbili ndizo za maana kutajwa. Kwanza, sheria kwa kweli iliwazaidia maskini kufanya hali yao isiwe mbaya. Ingekuwa vipaya kuingia katika umasikini na ingekuwa jambo la kuaibisha kutafuta usaidizi. Lakini ikiwa juu ya kulipa mkopo, mtu maskini aliitajika kulipa riba, jukumu ambalo lilikuwa la kufedhehesha sana kuliko lizaidie.
Pili, sheria ilifunza somo la maana sana kiroho. Kwa mkopeshaji kutolipisha riba kwa mkopo kwa mtu lingekuwa tendo la ukarimu. Atapoteza hizo pesa zilipokuwa kwa mikono mingine. Vile vile hiyo itakuwa njia ya ushahidi ya kudhihirisha shukrani kwa Mungu kwa huruma zake ambazo halipishi watu wake kama “riba” kwa neema ambayo ameifikisha kwao. Kama vile Mungu kwa huruma zake aliwatoa Waisraeli katika Misri wakati hawakuwa kitu cho chote na kuwa watumwa alikwisha wapa nchi ambayo ni yao (Mambo Ya Walawi 25:38), kwa hivyo aliwatarajia waonyeshe ukarimu huo huo kwa raia wenzao maskini.
Wakristo wako katika hali sambamba kama hiyo. Maisha, kifo na kufufuka kwa Yesu kumetulipia deni ya dhambi zetu kwa Mungu. Sasa, vile tunapokuwa na nafasi tuwazaidie wengine, hasa wale ambao ni Wakristo, kwa mikopo ambazo haziwezi ongeza shida zao. Yesu hata alitoa mfano unayohusiana na mambo haya kuhusu wadeni wawili na nia yao juu ya kusamehe (Mathayo 18:23-35).
Bibilia vile vile haikatazi au kuhukumu kukopesha pesa. Hekima ya Bibilia yatufunza kwamba kila mara si hoja nzuri kuingia katika deni. Deni hasa hutufanya kuwa mtumwa kwa yule anayetupa mkopo. Kwa wakati huo huo, katika hali zingine kuingia katika deni “dhambi ya lazima.” Vile pesa zinavyo tunzwa kwa hekima na malipo ya madeni yamedhibitiwa, Mkristo anaweza kuchukua mzigo wa deni ya kifedha kama hiyo italazimu.
No comments: