Ubatizo wa kikristo una umuhimu gani?”
Jibu: Ubatizo wa kikristo, kulengana na Biblia, ni ushahidi wa nje wa yale yaliyotendeka ndani ya maisha ya mwenye kuamini. Ni mfano wa kufa kwake kristo, kuzikwa na kufufuka kwake. Biblia inasema, ‘ ama hamjui kuwa sote tuliobatizwa katika kristo Yesu tulibatizwa katika kifo chake? Hivyo tulizikwa pamoja naye kupitia ubatizo katika wafu na kama kristo alivyofufuka kwa utukufu wa Mungu nasi tuishi maisha mapya” (warumi 6:3-4 ). katika ubatizo wa kikristo tendo la kuzamishwa ndani ya maji linaashiria kuzikwa na kristo. Tendo la kuzuka kutoka ndani ya maji lina maana ya kufufuka kwa kristo.
Katika ubatizo wa kikristo, kuna masharti mawili kabla mtu kubatizwa: (1) mwenye kubatizwa lazima awe amemwamini Yesu kristo kama mwokozi na (2) lazima abatizwaye afahamu umuhimu wa ubatizo huo. Kama mtu ana mtambua Yesu kristo kama mwokozi wake na ana ufahamu juu ya maana halisi ya ubatizo wa kikristo, kama njia ya heshima ya kudhihirisha wazi wazi imani yake juu ya kristo, akitaka kubatizwa hakuna pingamizi yoyote. Kulengana na Biblia, ubatizo wa kikristo ni muhimu kwa sababu ni hatua ya heshima- kudhihirisha waziwazi imani yako juu ya kristo na kuwajibika kwako kumfuata yeye kwa kujitambulisha naye katika kufa kwake, kuzikwa na kufufuka.
No comments: