Latest News


More

IBADA YA SHUKURANI YA WAZEE WA DAYOSISI YA MASHARIKI NA PWANI YAFANYIKA USHARIKA WA MBEZI BEACH

Posted by : Unknown on : Sunday, October 12, 2014 0 comments
Unknown
 Jana jumamosi katika Usharika wa Mbeze Beach wazee wastaafu na wapya wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani walifanya ibada maalum ya kumshukuru Mungu kwa kumaliza salama vipindi vyao (kwa wale waliostaafu) na kumshukuru Mungu kwa kuchaguliwa kuongoza watu wa Mungu kwa viongozi wapya
Ibada hiyo ilihudhuriwa na viongozi takriban wote wa Dayosisi wakiongozwa na Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ambaye pia ni askofu wa dayosisi hiyo Dr Alex Gerhaz Malasusa.
Pamoja na viongozi wakuu wa Dayosisi pia walikuwepo baadhi ya wachungaji wa sharika mbalimbali na baadhi ya viongozi wa huduma ambazo ziko chini ya dayosisi hiyo kama vile Maendeleo Bank, Mtoni Diaconia Center, chuo kikuu cha Tumaini, Pendo Redio Nk
Pichani juu mkuu wa kanisa la K.K.K.T Askofu Dr Alex Malasusa akihubiri kwenye ibada hiyo
Baadhi ya wazee waliohudhuria ibada hiyo ya shukrani wakiwa kwenye ibada
















No comments:

Leave a Reply