Latest News


More

MTU MWINGINE APATIKANA NA UGONJWA WA EBOLA MAREKANI

Posted by : Unknown on : Sunday, October 12, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :

Mfanyikazi mwengine wa kituo cha afya aliyemtibu Thomas Dancun kabla ya kifo chake katika jimbo la Texas nchini Marekani amepatikana na virusi vya ugonjwa wa Ebola.
''Tulijua kuna uwezekano wa kisa cha pili kuripotiwa ,na tumejitayarisha kwa uwezekano huo''alisema Daktari David Lakey ambaye ni kamishna wa idara ya afya katika jimbo la Texas.
Marehemu Dancun ambaye aliambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia ,alifariki katika hospitali ya Dallas siku ya jumatano.
Hatahivyo jina la muhudumu huyo halikutajwa.
Bwana Duncan alipatikana na virusi vya ugonjwa huo katika mji wa Dallas mnamo tarehe 30 mwezi Septemba ,siku kumi baada ya kuwasili kutoka katika ndege ya Monrovia kuelekea Brussels.
Aliugua siku chache baada ya kuwasili nchini Marekani,na kuelekea katika hospitali ya Texas mjini Dallas akiwa na homa kali.
Lakini licha ya kuwaeleza madaktari kwamba alisafiri kutoka nchini Libya,aliagizwa kwenda nyumbani baada ya kupewa dawa za maumivu.

Lakini Duncan baadaye aliwekwa katika karantini katika hospitali hiyo ,na kufariki baadaye licha ya kupewa dawa za majaribio.

Haijulikani iwapo afisa huyo aliyepatikana na virusi vya ugonjwa huo alikaribiana na Duncan au la baada ya kuonyesha dalili ama wakati alipolazwa hospitalini.
Afisa huyo alipatikana na homa siku ya ijumaa kabla ya kuwekwa katika karantini ili kufanyiwa ukaguzi.

No comments:

Leave a Reply