Latest News


More

Mtu anawezaje kuwa mzazi bora?

Posted by : Unknown on : Thursday, March 26, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :

Mtu anawezaje kuwa mzazi bora?

Je, unamfundisha mtoto wako kumpenda mungu?
Familia ambayo wazazi wanapendana na kuheshimiana ni msingi mzuri wa malezi bora kwa mtoto. (Wakolosai 3:14, 19) Wazazi bora huwapenda na kuwapongeza watoto wao, kama vile Yehova alivyompongeza Mwana wake.—Soma Mathayo 3:17.
Baba yetu wa mbinguni husikiliza na kukazia fikira hisia za watumishi wake. Ni jambo linalofaa kwa wazazi kumwiga kwa kuwasikiliza watoto wao wanapozungumza. (Yakobo 1:19) Wanahitaji kuelewa hisia za watoto wao, kutia ndani zile ambazo huenda hazifai.—Soma Hesabu 11:11, 15.

Unawezaje kuwalea watoto wawe wenye kutegemeka?

Ukiwa mzazi una mamlaka ya kuweka sheria. (Waefeso 6:1) Jifunze kutokana na mfano wa Mungu. Huwaonyesha upendo watoto wake kwa kueleza waziwazi sheria na kueleza matokeo ya kutozitii sheria hizo. (Mwanzo 3:3) Pia, badala ya kuwalazimisha watu kumtii, anawafundisha jinsi watakavyofaidika kwa kufanya mambo yaliyo sawa.—Soma Isaya 48:18, 19.
Fanya iwe lengo lako kuwasaidia watoto wako wampende Mungu. Kisha, watatenda kwa hekima hata watakapokuwa peke yao. Kama Mungu anavyofundisha kwa kuweka mfano, wafundishe watoto wako kumpenda Mungu kwa kuwawekea mfano.—Soma Kumbukumbu la Torati 6:5-7; Waefeso 4:32; 5:1.

No comments:

Leave a Reply