Latest News


More

WAWEZAJE KUSHUGHULIKA NA MTOTO MWENYE MLIPUKO WA HASIRA

Posted by : Unknown on : Thursday, April 23, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :


Jinsi ya Kushughulika na Mtoto Mwenye 

Mtoto wako mwenye umri wa miaka miwili anapokasirika, anaanza kupiga kelele, anapiga-piga miguu chini kwa kishindo, na anajigaragaza chini. Unajiuliza: ‘Mtoto wangu yuko sawa kweli? Je, analipuka kwa hasira kwa sababu nimekosa kumtimizia mahitaji yake? Je, atawahi kuacha tabia hii?’
Unaweza kumsaidia mtoto wako mwenye umri wa miaka miwili abadili tabia yake. Lakini, kwanza, fikiria tabia hiyo inasababishwa na nini.

KWA NINI HILI HUTUKIA

Watoto wadogo hawana uwezo wa kudhibiti hisia zao. Hali hiyo pekee inaweza kuwafanya walipuke kwa hasira mara kwa mara. Hata hivyo, kuna sababu nyingine.
Fikiria mabadiliko ambayo mtoto anapitia anapokuwa na umri wa miaka miwili hivi. Tangu alipozaliwa, wazazi wake walimfanyia kila kitu. Kwa mfano, alipolia, wazazi walikuja haraka. ‘Je, mtoto anaumwa? Je, ana njaa? Je, anahitaji kubembelezwa au kubadilishwa nepi?’ Wazazi walifanya chochote kilichohitajiwa ili kumtuliza mtoto wao. Ilikuwa sawa kufanya hivyo kwa sababu mtoto anawategemea kabisa wazazi wake kwa kila kitu.
Hata hivyo, anapofikia umri wa miaka miwili hivi, mtoto anaanza kutambua kwamba wazazi wake hawafanyi tena mambo anayotaka wamfanyie. Kwa kweli, badala ya wao kumtimizia matakwa yake, wanatazamia yeye atii matakwa yao. Sasa mambo yamebadilika, na mtoto wa umri wa miaka miwili hatakubali mabadiliko hayo kwa urahisi—huenda akalipuka kwa hasira.
Baada ya muda, kwa kawaida mtoto anakubaliana na ukweli wa kwamba wazazi wake si watunzaji wake tu bali pia ni wafundishaji wake. Inatumainiwa pia kwamba baadaye atatambua kuwa jukumu lake ni ‘kuwatii wazazi wake.’ (Wakolosai 3:20) Kwa sasa, huenda mtoto akawafanya wazazi washindwe kabisa kuvumilia milipuko yake ya hasira.

 MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA

Elewa hali yake. Mtoto wako si mtu mzima. Kwa kuwa hajui jinsi ya kushughulika na hisia zake, anaweza kukasirika sana anapofadhaika. Jaribu kuona mambo kama yeye anavyoyaona.—Kanuni ya Biblia: 1 Wakorintho 13:11.
Uwe mtulivu. Mtoto wako anapolipuka kwa hasira, kukasirika hakutakusaidia. Kwa kadiri inavyowezekana, puuza mlipuko wake wa hasira na udhibiti hisia zako. Kukumbuka kwa nini milipuko ya hasira hutokea kutakusaidia kuwa mtulivu.—Kanuni ya Biblia: Methali 19:11.
Shikilia msimamo wako. Ikiwa unampa mtoto wako kila kitu anachotaka kwa sababu tu analipuka kwa hasira, yaelekea ataendelea kufanya hivyo kila mara anapotaka kitu fulani. Kwa utulivu mwonyeshe mtoto wako kwamba hutalegeza msimamo wako.—Kanuni ya Biblia: Mathayo 5:37.
Kukumbuka kwa nini milipuko ya hasira hutokea kutakusaidia kuwa mtulivu
Uwe na subira. Usitazamie kwamba mtoto wako ataacha mara moja tabia ya kulipuka kwa hasira, hasa ikiwa umempa sababu ya kuamini kwamba akilipuka kwa hasira utamruhusu afanye chochote anachotaka. Hata hivyo, ikiwa unashughulikia hali kwa njia inayofaa na bila kuwa kigeugeu, yaelekea milipuko ya hasira itapungua. Hatimaye, itaisha kabisa. Biblia inasema: “Upendo ni wenye ustahimilivu.”—1 Wakorintho 13:4.
Pia jaribu mambo yafuatayo:
  • Mlipuko wa hasira unapoanza mshikilie mtoto wako (ikiwa inawezekana) na, bila kumwumiza, mzuie asijigaragaze. Usimfokee mtoto wako. Subiri tu mpaka hali itulie. Hatimaye, mtoto atatambua kuwa kulipuka kwa hasira hakukumsaidia kwa njia yoyote.
  • Tenga mahali utakapomweka mtoto wako anapolipuka kwa hasira. Mwambie kwamba atatoka humo mara tu anapotulia, na kisha umwache humo.
  • Ikiwa mtoto wako analipuka kwa hasira mbele za watu, mwondoe hapo. Usimpe anachotaka eti kwa sababu tu amelipuka kwa hasira mbele za watu. Ukimpa, hilo linaweza kufanya afikiri kwamba ikiwa atalipuka kwa hasira, anaweza kupata chochote anachotaka.

No comments:

Leave a Reply