Katika ibada hiyo Bwana Ngowi alisema hili ni wiki la kujisomea Biblia ambalo dhumuni kubwa la umoja huo ni pamoja na;
1.Kufanya kazi ya kueneza injili kwa watu wote hususan watoto na vijana
2.Kuhamashisha wakristo kusoma Biblia
3.Kuendesha semina na makongamano kwa vijana na watoto na vipindi vya dini mashuleni
4.Kuendesha semina za ndoa
5.Kutoa ushauri nasaha na wa kitaalam, kiroho na kielimu
6.Kuendesha na kusimamia chama cha wanahabari wa kikristo Tanzania
Pia bwana Ngowi alisema kuwa mtu yoyote anaweza kushirikiana nao kwa;
1.Kwa njia ya maombi
2.Kujiunga na kuwa mwanachama
3.Kama mtu ana wito wa kuhubiri injili anaweza pia kujiunga nao
4.Kuuza na kusambaza kazi mbalimbali kama vitabu na vipeperushi
Neno kuu la wiki hii ya Kujisomea Biblia linatoka 1 Samw.1:1-20
somo ambalo alisoma mtumishi huyo linatoka 2 Kor 9:6-11
Yesu akasema atakayemtumikia na Baba wa mbinguni atamheshimu
-Hivyo ukitaka kuheshimiwa na Mungu uwe tayaru kumtumikia
- Utoaji ni njia mojawapo ya kumtumikia Mungu
Katika somo hiilo mtumishi huyo alisisitiza kuwa Biblia inasema kuwa;
1.Apandaye haba ahavuna haba, na ukipanda kwa ukarimu utavuna kwa ukarimu
2.Kila mtu atende kama alivyo kusudia moyoni mwako.i kwa huzuni wala kwa kulazimishwa
3.Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu.Usitoe kwa huzuni au kwa malalamiko
4.Mungu ndiye atoaye mbegu na yeye mwene kupanda; na Mungu ndiye anayezidisha
Zab 24: 1 - Nchi na vyote ni mali ya Bwana;Dunia na wote wakaao ndani yake..Kol 1: 15-16
5.Yesu ni mfano wa Mungu asiyeonekana na ni mzaliwa wa kwanza - Ukimwona Yesu umemwona Mungu - 2 Kor 8:1-5
6. Unaupata utajiri kwa sababu ya ukarimu wako/utoaji wako kwa Mungu
7. Toa kwa hiari yako mwenyewe
- Hakuna ulinzi wa milele kwa shetani ..Yoha 10:10 lakini kwa Yesu kuna ulinzi wa milele
8. Shetani hapendi usome/ujue neno la Mungu Yoh 8:31-36
Mama Chonjo naye akiwa kwenye ibada hiyo ambayo ilikua ni maaluma kwa ajili ya kusifu na kuabudu
Washarika wakifuatilia ibada hiyo ya jumapili
Mzee Kihundwa (ambaye ni mzee wa kanisa wa ibada ) akisoma matangazo ya Usharika
Waumini wakifuatilia ibada hiyo
No comments: