Bi Sakina akiwasili nyumbani kwa wazazi wake
Ndugu na marafiki wa bwana harusi wakiwa nyumbani kwa wakwe zao
Kaka wa bwana harusi Bwana Riziki akisalimiana na babu wa bi Sakina mara baada ya kuwasili nyumbani hapo
Mama wa bi Sakina akiwa na ndugu zake wakiwapokea wageni wao mara baada ya kuwasili
Bwana Rahima akiwa na mke wake bi Sakina na mpambe wa bwana harusi bwana Kitwana wakiwa nyumbani kwa wakwe zake
Wakina mama wakipokea baadhi ya vitu walivyokuja navyo siku hiyo ikiwa ni pamoja na mbuzi na kuku kwa mujibu wa mila za Kibondei
Mzee wa mila akitengeneza baadhi ya vifaa ambavyo vinatumika kupokelea baadhi ya mahari.Pichani ni bwana Riziki (kaka wa bwana harusi), mzee wa mila katikati na bwana Kichila wakifuatilia matengenezo hayo
Mzee wa mila akitoa maelezo ya baadhi ya vitu vilivyoletwa siku hiyo
Baada ya kupokea sehemu ya mahari kiliandaliwa chakula rasmi kwa ajili ya bwana harusi na marafiki zake maarufu kama Kombe
Bwana harusi akipakua kombe kwa ajili ya kupeleka kwa mke wake bi Sakina
Marafiki zake na bwana harusi wakinawishwa mikono tayari kula kombe.
Baada ya kula walinawishwa mikono
Bada ya kula ilipigwa dua na ustaadhi .Kutoka kulia ni bwana Kitwana, Bwana harusi Rahim. bwana Peter Mkasimongwa na ustaadhi alieendesha dua hiyo
No comments: