Jibu:
Una njaa? Si njaa ya chakula, lakini je, una njaa ya kitu Fulani zaidi
maishani? Je, kuna hali Fulani ya kutotosheka ndani yako? Ikiwa iko basi Yesu
ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mkate wa kweli. Kila ajaye kwangu hatahisi
njaa na aniaminiye hataona kiu” (Yohana 6:35).
Je, umechanganyikiwa? Je,
huoni mbele ya maishani mwako? Je, unajihisi kama umeachwa kwenye giza na huoni
pa kutokea? Ikiwa hali yako ni kama hiyo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema,
“Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. Anifuataye hatatembea gizani, bali atakuwa na
nuru ya uzima” (Yohana 8:12).
Je, unajisikia kama umefungiwa nje ya
maisha yako? Je, umejaribu njia nyingi na kutambua ya kwamba kile
ulichokitarajia hakipo ndani yake? Je, unatafuta njia ya kufikia maisha
makamilifu? Ikiwa haya ndiyo uyatafutayo, Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi
ndimi mlango wa kondoo; aingiaye kupitia mimi ataokolewa. Ataingia na kutoka na
kupata malisho” (Yohana 10:9).
Je, watu wengine husababisha kushindwa
kwako? Je, uhusiano wako nao umekuwa si wa kina na bila muelekeo? Je, ni kama
watu wanakutumia tu kwa manufaa yao? Ikiwa ndiyo hali unayopitia Yesu ndiye
njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa uhai wake
kwa ajili ya kondoo……. Mimi ndimi mchungaji mwema; Ninajua kondoo wangu na
kondoo wangu wananijua” (Yohana 10: 11,14).
Je, unashangazwa na
kinachotendeka baada ya maisha haya? Je, umechoshwa na maisha ya kupigania tu
vitu vinavyooza na kushika kutu? Je, wakati mwingine maana ya maisha yako
huionea shaka? Je, unataka kuishi hata baadaya kufa? Ikiwa haya ndiyo uliyonayo
basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Aniaminiye
ataishi, hata ajapokufa; na aishiye na kuniamini hata kufa kamwe”
(Yohana11:25-26).
Njia ni nini? Ukweli ni nini? Uzima ni nini? Yesu
akajibu, “Mimi ndimi njia kweli na uzima.Hakuna afikaye kwa baba bila kupitia
kwangu” (Yohana 14:6).
Njaa unayoihisi ni njaa ya kiroho, na inaweza
kutoshelezwa na Yesu. Yesu ndiye pekee anaweza kuondoa giza maishani mwako. Yesu
ndiye mlango wa maisha ya kutosheka. Yesu ndiye rafiki na mchungaji uliyekuwa
ukitafuta. Yesu ndiye uzima wa ulimwengu wa sasa na ujao. Yesu ndiye njia ya
wokovu!
Unahisi njaa, kujisikia kama uliyepotea gizani na maisha yako
kukosa maana kwa kuwa umetengana na Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba sote
tumetenda dhambi na kutengana na Mungu (Mhubiri 7:20; Warumi 3:23). Kujihisi
kuwa maisha yako hayana maana ni kwa kutokuwepo kwa Mungu maishani mwako.
Tuliumbwa tuwe na uhusiano na Mungu. Kwa sababu ya dhambi zetu tumetengwa nje ya
uhusiano huo. Vibaya zaidi ni kwamba dhambi zetu zitasababisha kutengwa sasa na
hata baada ya ufufuo, milele (Warumi 6:23; Yohana 3:36).
Shida hii
inawezaje kutatuliwa? Yesu ndiye njia! Yesu alichukua dhambi zetu (wakorintho wa
pili 5:21). Yesu alikufa kwa ajili yetu (Warumi 5:8), akachukua adhabu
iliyotupasa sisi. Siku tatu baadaye, yesu akafufuka kutoka kwa wafu kuthibitisha
ushindi wake juu ya dhambi na mauti (Warumi 6:4-5). Kwa nini alifanya hivyo?
Yesu alijibu swali hilo mwenyewe, “Upendo mkuu hakuna mwingine mwenye nao kama
huu, kwamba atoe uhai wake kwa ajili ya rafiki” (Yohana 15:13). Yesu alikufa ili
tupate kuishi. Tukiweka imani zetu ndani ya yesu tukiamini kufa kwake kuwa fidia
ya dhambi zetu – dhambi zetu zote zinasamehewa na kufutwa. Atahakikisha njaa
yetu imetoshelezwa. Mataa ya kimaisha yataangaza tena. Tutapata nafasi ya
kufikia maisha ya utimilifu. Tutamjua rafiki yetu mwema na mchungaji pia.
Tutajua ya kwamba tutaishi tena hata baada ya kufa – maisha baada ya ufufuo
mbinguni milele na Yesu!
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu
hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa
milele” (Yohana 3:16).
No comments: