Latest News


More

ASKOFU MUNGA AHIMIZA UWEKEZAJI ELIMU YA JUU NCHINI

Posted by : Unknown on : Monday, December 30, 2013 0 comments
Unknown

Lushoto. Askofu wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Dk Stephen Munga, amezungumzia umuhimu wa Tanzania kuwekeza katika elimu ya juu na kwamba kuwa taifa lolote lisilowekeza katika elimu litakuwa taabani kimaendeleo hasa ya kiuchumi.
“Taifa lolote ambalo halitatazama elimu kama nyenzo ya kujenga utamaduni wa kuleta mabadiliko ya fikra kwa ajili ya maendeleo ya watu wake, liko taabuni,” alisema Dk Munga.
Kiongozi huyo wa kidini, alikuwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (Sekomu). Dk Munga ambaye ndiye mkuu wa kwanza wa chuo hicho, alisisitiza juu ya haja ya taifa kuthamini elimu ya vyuo vikuuu, ambavyo aliviita kuwa ni viwanda vya fikra na maarifa mapya.
Hata hivyo, alitahadharisha kuwa uwekezaji katika elimu lazima uzingatie upana wa fursa katika watu kupata elimu. “Elimu lazima iwe na viwango vifaavyo ili kunufaisha wanaoipata na jamii itakayohudumiwa kwa maarifa yaliyopatikana kwa njia ya elimu hiyo,” alisema.
Dk Munga alisema ingawa Serikali inajitahidi kufanya hayo, bado kuna mambo mengi yanayostahili kufanywa kulingana na ushauri wa wataalamu mbalimbali.
Mkuu huyo wa chuo alisema wakati umefika kwa Serikali kuona haja ya kufanya ukarabati mkubwa wa mfumo mzima wa elimu ikiwa ni pamoja na kuona uwezekano wa kuwapa mikopo wanafunzi wote Watanzania wanaojiunga na elimu ya juu.
Alisema kanisa limeanzisha chuo kikuu hicho kwa lengo la kuchangia ujenzi wa utamaduni wa kupata na kurithishana maarifa yenye malengo ya kuboresha maisha ya watu.

No comments:

Leave a Reply