IBADA YA MWISHO WA MWAKA KATIKA KANISA LA K.K.K.T – USHARIKA WA MWENGE
Mungu anapenda watu wanaomtii na kumpenda yeye.Akihubiri katika ibada ya mkesha wa mwaka mpya jana usiku mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge wa Kanisa la K.K.K.T Mchungaji Kaanasia Msangi alisema Wayahudi waliamini kwamba Mungu (Yehovah) ndiye Mungu mkuu
Akisoma neon toka Kumb.6: 4 – 7 alisema somo linazungumzia mambo makubwa mawili ambayo ni;
1.Kumpenda Mungu
2.Kumtii Mungu
Kupitia kitabu cha kumbukumbu Mungu aliwakumbusha Wayahudi kwamba kama hawatatii maneno yake, wasahau kabisa upendeleo wake katika urithi wa Uzima wa milele
Mungu aliwataka watembee na kuishi kwa sheria zake alizowapa na amri zake
Yesu Kristo anasema “Mkinipenda , mtazishika amri zangu”
Hata leo Mungu anatutaka tuzitii na kuzishika amri zake alimalizia mchungaji Kaanasia Msangi
Katika ibada hiyo ilihudhuriwa na waumini wengi na kuongozwa na vikundi mbalimbali vya kwaya vya usharika huo
No comments: