Mwimbaji wa kujitegemea Joshua Mlelwa maarufu kama Brother Joshua jumapili ya leo ameongoza ibada ya kusifu na kuabudu iliyofanyika katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge
Katika ibada hiyo iliyoanza saa moja na nusu na kuongozwa na mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge ,mchungaji Kaanasia Msangi akisaidiana na mchungaji Erasto Shaila
Pia kulikua na vikundi vya kwaya nya Usharika huo kama vile kwaya ya Uinjilisti, kwaya kuu, kwaya ya vijana wa Alpha Sekondari, kwaya ya akina mama na kikundi cha Praise and worship Team cha usharika huo
Pichani juu brother Joshua akiimba kwa hisia na nyuma yake ni waimbaji wa praise team wa Usharika wa Mwenge
Mkewe Joshua Mlelwa wa pili toka kulia akiimba na waimbaji wa Praise and worship team wa Mwenge
No comments: