Latest News


More

TUKIMTEGEMEA YESU TUTASHINDA MAJARIBU

Posted by : Unknown on : Sunday, March 9, 2014 0 comments
Unknown


Neno Kuu Mathayo 4:1-10
Neno la waraka Yakobo 1:12-18
Zaburi 91 1:10

Mungu ndiye mkuu wa mambo yote hapa duniani, na hakuna kinachomshinda yeye, hivyo hata sisi tukimtegemea yeye hakuna kitakachotushinda
Akihubiri katika ibada ya jumapili hii ya leo mama Kihundwa (pichani juu) alisema majaribu ni mfumo
na ibilisi shetani na alianza kwa kumjaribu Adam na Hawa pale katika bustani ya Edeni.
Lakini pia Yesu kristo alipitiamajaribu mengi katika uhai wake hapa dunuani.Baada ya Ubatiso Yesu aliongozwa na Roho Mtakatifu hadi jangwani alikokaa  siku 40 mchana na usiku bila ya kunywa wala kula
Yesu Kristo alipitia majaribu mengi lakini biblia inaeleza majaribu makuu matatu ambayo ni;
1.Shetani alimwambia Yesu aamuru mawe kuwa mikate akijua kwamba Yesu Kristo alikua na njaa sana
2.Shetani alimwambia Yesu Kristo ajitupe chini toka kwenye mnara na malaika watamzuaia asianguke
3.Shetani alimwambia Yesu Kristo amsujudie ili ampe milki yote na mali yote iliyoko duniani
Akiendelea kuhubiri katika ibada ya asubuhi mama Kihundwa alisema tunajifunza nini katika majaribu ya bwana Yesu Kristo
1.Jaribu la kwanza, ibilisi alitumia kigezo cha njaa.Ibilisi alijua kwa kua Yesu alikua na njaa akitumia kigezo hicho atamhadaa, bila kujua kwamba Yesu Kristo alijaa Roho mtakatifu ndani yake.
Swali tunaloweza kujiuliza sisi ni kwamba sisi kama wakristo tunaweza kuhimili njaa pale tunapojaribiwa?
2.Shetani alitumia kigezo cha kifo kwa kujua kwamba kila mwanadamu anaogopa kifo bila kujua kwamba Yesu Kristo alikua Mungu  na mwanadamu pia.Hata sisi binadamu wa leo tunaogopa kifo
3.Ibilsi alitumia kigezo cha mali .Hakuna binadamu asiyependa mali, hivyo shetani alijua akitumia kigezo hicho ni rahisi kumtega bila kujua kwamba mbingu na nchi na vyote vilivyopo duniani ni mali ya Munguna hakuweza kumtia majaribuni
Hivyo tunaona kuwa Yesu alishinda majaribu kwa kuwa;
1.Yeye ni Mungu
2.Aliongozwa na Roho mtakatifu na kwa kua neon lilikua ndani yake
Hata sisi wakristo wa leo tunaweza kushinda majaribu kwa kumtegemea roho mtakatifu na mali na ukuu si chochote kwetu kama tunaye Roho Mtakatifu alimaliza mama Kihundwa


Usharika wa Mwenge Suzane Mwimbe akisoma neno la waraka

Mama Seka Urio akisoma matangazo ya Usharika Mama Urio na wenzake walisaidiana huduma kama wazee wa zamu katika ibada hiyo

Pichani juu washarika wakiwa kwenye ibada hiyo ya jumapili
Ibada hiyo iliongozwa na wanawake peke yao .Mwongozaji wa ibada alikua mama Rose Matogolwa

No comments:

Leave a Reply