Pasaka
ilianza lini na nani?, Inamaanisha nini?
Kutoka 12:1
BWANA akanena na Musa, na
Haruni katika nchi ya Misri akawaambia, ”Mezi huu utakuwa mwanzo wa miezi kwenu; utakuwa ni mwezi wa kwanza wa
mwaka kwenu”
Kumbukumbu
la Torati 16:1 Na ndiyo sheria, na amri, na hukumu, alizoziamuru BWANA, Mungu
wenu, mfundishwe, mpate kuzitenda katika nchi ile mnayoivukia kuimiliki;
Tangu wakati wa
kuanzishwa kwa Sheria za Musa, utaratibu wa kuhesa miezi uliojulikana kwa
Wayahudi ulikuwa ni ule wa Miandanmo ya Mwezi lakini ilihusiana na mwelekeo wa
machweo ya jua. Utaratibu wa mzunguko hadi kufikia siku za maadhimisho ya
sikukuu za kidini ilitegemea sana na miandamo ya mwezi. Mwaka wa kidini ulianza
katika kipindi kinachokaribiana na kile cha usiku na mchana kuwa na muda sawa
katika mzunguko wa jua linapopita katikati ya mstari wa Ikweta, yapata kama
tarehe 21 Marchi. Utaratibu wa kuhesabu mwanzo wa mwezi ulianzia na mwandamo wa
mwezi mpya. Kwa maneno mengine ni kwamba ulianzia katika maadhimisho ya
mwandamo wa mwezi mpya kwa maneno mengine ni kwamba, mwaka ulianzia katika
muandamo wa mwezi mpya uliofuatia mwanzo wa majira ya baridi. Kuna mambo
yakupendeza kuyajua kuhusiana na hali hii. Inaonekana kwamba dunia iliumbwa
katika kipindi hiki cha majira ya baridi wakati wa kipindi kile cha Uumbaji.
Pia baada ya gharika kuu, Nuhu alifungua mlango wa Safina na kutoka kuanza
maisha mapya kwenye Ulimwengu Mpya katika kipindi hiki cha baridi cha mwaka
ule. Wana wa Israeli pia walitoka kutoka nchi ya utumwa ya Misri katika kipindi
hiki hiki cha majira ya baridi. Kipindi hiki cha majira ya baridi ni cha
kufanywa tena kwa mambo yote katika asili zake, ni ishara ya uumbaji mpya wa
Mungu wa maisha mapya. Mwezi huu wa Abibu hatimaye ulijulikana kama mwezi wa Nisani
Kutoka 12: 3 ”Semeni na
mkutano wote wa Israeli, mkawambie, Siku ya kumi ya mwezi huu kila mtu atatwaa
mwana kondoo, kwa hesabu ya nyumba ya baba zao, mwana kondoo, kwa hesabu ya
nyumba ya baba zao, mwana kondoo kwa watu wa nyumba moja;
4 na ikiwa watu wa nyumbani
niwachache kwa mwana kondoo, basi yeye na jirani yake aliye karibu na nyumba
yake na atwae mwana kondoo mmoja, kwa kadiri ya hesabu ya watu; kwa kadiri ya
ulaji wa kila mtu, ndivyo mtakavyofanya hesabu yenu kwa yule mwana kondoo.
5 Mwana kondoo wenu atakuwa
hana ila, mume wa mwaka mmoja; mtamtwaa katika kondoo au katika mbuzi.
6 Nanyi mtamweka katika siku
ya kumi na nne ya mwezi ule ule; na kusanyiko lote la mkutano wa Israeli
watamchinja jioni
Kuanzia mwanzoni
kabisa mwa uumbaji Mungu alitupa ishara ili kutufanya sisi tuitambue zawadi
yake ya upatanisho ambayo ni huyu Mwana wake wa pekee Yesu Kristo. Katika
uumbaji wake aliiumba mianga mikuu miwili ambyo ni Jua na Mwezi, ambavyo
vinawakilisha Kristo na Kanisa. Aliviumba siku ya nne ya juma la uumbaji (2
Petro 3:8 inasema ….). Pia kwenye Pasaka yule Mwana Kondoo alitunzwa
na kuhifadhiwa kwa muda wa siku nne. Katika siku ya miaka-elfu nne, Kristo na
kanisa walizaliwa.
Kutoka 12: 7 – 8
”Nao
watatwaa baadhi ya damu yake na kuitia katika miimo miwili na katika kizingiti
cha juu, katika zile nyumba watakazomla. Watakula
nyama yake usiku ule ule, imeokwa motoni, pamoja na mkate usiotiwa chachu; tena
pamoja na mboga zenye uchungu”
Huu ni mfano wa
mana ambayo kwayo Kristo alikufa. Taji la miiba na misumari aliyopigiliwa
mikononi mwake, yote iluimchoma mwili wake na alkufa msalabani. Damu ilipakwa
kwenye miimo ya milango kwenye hali sawa na ile damu iliyomwagika msalabani.
Uchungu
Uchungu ni
dalili ya mateso, kutendewa ukatili na utumwa kama tusomavyo Kutoka
1:14, Warumi 1:20 na Yeremia 9:15. Pasaka iliambatana na kula "mboga za
uchungu", Kutoka 12:8, Hesabu 9:11. Hii mboga iliyoliwa hapa
haijulikani ilikuwa ni ya aina gini. Huenda ilikuwa ni aina yoyote ya mboga
chungu iliyopatikana mahali pale walipokuwa na iliyopatikana kipindi ambacho
Pasaka ilikuwa inaadhimishwa. Mboga hii iliwakilisha taswira ya uchungu wa
utumwa ambapo watu walitaabishwa kwao; na inachukuliwa pia kuwa ni taswira ya
mateso ya Kristo.
Kutoka 12:9 – 25
”Msiile
mbichi, wala ya kutokoswa majini, bali imeokwa motoni; kichwa chake pamoja na
miguu yake, na nyama zake za ndani. Wala msisaze kitu chake cho chote hata
asubuhi, bali kitu kitakachosalia hata asubuhi mtakichoma kwa moto. Tena mtamla
hivi; mtakuwa mmefungwa viuno vyenu, mmevaa viatu vyenu miguuni, na fimbo zenu
mikononi mwenu; nanyi mtamla kwa haraka; ni pasaka ya BWANA. Maana nitapita
kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote wa
mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi
ndimi BWANA. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika zile nyumba mtakazokuwamo;
nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu, lisiwapate pigo lolote
likawaharibu, nitakapoingia nchi ya Misri. Na siku hii itakuwa ukumbusho kwenu,
nanyi mtaifanya iwe sikukuu kwa BWANA; mtaifanya iwe sikukuu katika vizazi
vyenu vyote, kwa amri ya milele. Hapo ndipo Musa akawaita wazee wa Israeli,
na kuwaambia, Nendeni mkajitwalie wana-kondoo kama jamaa zenu zilivyo,
mkamchinje pasaka. Nanyi twaeni tawi la hisopo, mkalichovye katika ile damu
iliyo bakulini, na kukipiga kizingiti cha juu, na miimo miwili ya mlango, kwa
hiyo damu iliyo katika bakuli; tena mtu ye yote miongoni mwenu asitoke mlangoni
mwa nyumba yake hata asubuhi. Kwa kuwa BWANA atapita ili awapige hao Wamisri;
na hapo atakapoiona hiyo damu katika kizingiti cha juu, na katika ile miimo
miwili, BWANA atapita juu ya mlango, wala hatamwacha mwenye kuharibu aingie
nyumbani mwenu kuwapiga ninyi. Nanyi mtalitunza jambo hili kuwa ni amri
kwako na kwa wanao milele. Itakuwa, hapo mtakapoifikilia hiyo nchi, BWANA
atakayowapa, kama alivyoahidi, ndipo mtakapoushika utumishi huu”
[Tunapaswa
kuwa na meza iliyoandaliwa vizuri na sahani, bakuli na kikombe. Katikati ya
meza tunakuwa na sahani ya nyama iliyopambwa kwa saladi Maridadi na figili
zikiizunguka ile sahani lakini kukiwa tupu bila kuwepo nyama ndani yake.
(Kama tungeweka nyama kwenye hii sahani, basi tungehukumiwa kwa
kumsulibisha Kristo katika mwili kwa sababu yeye alikuwa ni ile sadaka
kamilifu iliyokomesha aina zote za dhabihu). Tunaanza kwanza kwa kula zile
mboga zenye uchungu (mchunga, ama aina yoyote ya mboga zenge uchungu za majani
lakini zisizo na madhara zikiliwa) zichovywe kwenye maji ya chumvi huku
tuliuliza maswali yafuatayo].
Maswali ya
Pasaka ni Yapi?
1. Je, ni kwa
nini usiku huu ni wa tofauti na nyingine zote?
Kutoka 12: 26 - 27
”Kisha
itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu?
Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba
za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu.
Hao watu wakainama vichwa na kusujudia”
2.
Je, ni kwa nini tunakula chakula hiki kisicho cha
kawaida?
Kutoka 1:13 – 14
”Wamisri
wakawatumikisha wana wa Israeli kwa ukali; wakafanya maisha yao kuwa machungu
kwa kazi nguvu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila namna ya kazi ya
mashamba’ kwa kazi zao zote walizotumikishwa kwa ukali.”
3. Je, ni kwa
nini tunachovya mboga hizi yenye uchungu kwenye maji machungu?
Kutoka 1:14
”Ili kuyakumbuka
machungu yaliyotokana na mateso ya utumwa ya Misri na jinsi walivyookolewa kwa
kupitia Bahari ya Shamu; wakafanya
maisha yao kuwa uchungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa nay a matofali, na kila
namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.”
4. Je, yuko wapi
Mwana kondoo wa Pasaka? Kwa kuwa sahani iko wazi.
Mwana Kondoo wa Dhabihu amekwisha
chinjwa tayari pale msalabani kwa hiyo teno la kuleta dhabihu kwenye sahani
lingemaanisha ni kumsulibisha Kristo kwa upya.
1 Wakoritho 5:7 – 8
”
Basi, jisafisheni, mkate ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama
vile mlivyo mahkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa
sadaka, yaani, Kristo; basi na tuifanye karamu, si kwa chachu ya kale, wala
kwa chachu ya uovu na ubaya, bali kwa yasiyochachika, ndio weupe wa moyo na
kweli.”
Waebrania 10:12 – 14
”Lakini huyu, alipokwisha kutoa kwa ajili ya dhambi
dhabihu moja idumuyo hata milele, aliketi mkono wa kuume wa Mungu; tangu hapo
akingojea hata adui zake wawekwe kuwa chini ya miguu yake. Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata
milele hao wanaotakaswa.”
(Hatuli
nyama kwenye ibada hii kwa sababu baada ya Kristo kusulibiwa ambaye ni
"Ddhabihu Kamilifu", basi tutakosea kama tutamchinja mnyama
tena. Hivyo basi tendo la sahani kuwa wazi inamaanisha kwamba Kristo
ndiye Mwana Kondoo wetu wa Pasaka).
Kutoka 12:26 – 39
”Kisha
itakuwa hapo watoto wenu watakapowauliza, N’nini maana yake utumishi huu kwenu?
Ndipo mtawaambia, Ni dhabihu ya pasaka ya BWANA, kwa kuwa alipita juu ya nyumba
za wana wa Israeli huko Misri, hapo alipowapiga Wamisri, akaziokoa nyumba zetu.
Hao watu wakainama vichwa na kusujudia. Hata ikawa, usiku wa manane BWANA
akawapiga wazaliwa wote katika nchi ya Misri, tangu mzaliwa wa kwanza wa Farao
aliyeketi katika kiti chake cha enzi, hata mzaliwa wa kwanza wa mtu aliyefungwa
katika nyumba ya wafungwa; na wazaliwa wa kwanza wote wa wanyama. Farao
akaondoka usiku, yeye na watumishi wake wote, na Wamisri wote; pakawa na
kilio kikuu katika Misri; maana hapakuwa na nyumba hata moja asimokufa mtu.
Akawaita Musa na Haruni usiku, akasema, Ondokeni tokeni katika watu wangu,
ninyi na wana wa Israeli; enendeni, mkamtumikie BWANA kama mlivyosema. Twaeni
kondoo zenu na ng’ombe zenu kama mlivyosema, enendeni zenu, mkanibariki mimi
pia. Wamisri nao wakawahimiza watu, kuwatoa katika nchi kwa haraka, maana
walisema, Tumekwisha kufa sote. Watu wakauchukua unga wa mikate yao kabla
haijatiwa chachu, na vyombo vyao vya kukandia wakavitia ndani ya nguo zao
mabagani. Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi mpaka Sukothi, walipata
hesabu yao kama watu sita mia elfu watu waume waliokwenda kwa miguu, bila
kuhesabu watoto. Na kundi kubwa la watu waliochangamana nao wakakwea pamoja
nao; na kondoo na ng’ombe, wanyama wengi sana. Nao wakaoka mikate isiyochachwa
ya ule unga waliochukua walipotoka Misri, maana, haukutiwa chachu, kwa sababu
walitolewa watoke Misri, wasiweze kukawia, nao walikuwa hawajajifanyia tayari
chakula.
Tunauvunja na kuula mkate usiotiwa chachu huku tukinywa juisi ya
zabibu. (Ni lazima iwe juisi
ambayo haikutiwa aina yoyote ya amira au iliyochachishwa kwa kuwa chachu
inawakilisha dhambi.) Wana wa Israeli waliamriwa kuondoa aina zote za chachu
majumbani mwao kipindi hiki.
Kristo
ambaye ndiye mfano wetu pia aliitunza sikukuu hii ya Pasaka.
Luka 22:7 – 20
”
Ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu, ambayo ilipasa kuchinja pasaka.
Akawatuma Petro na Yohana, akisema, Nendeni, mkatuandalie Pasaka tupate kuila.
Wakamwambia, Wataka tuandae wapi? Akawaambia, Tazama, mtakapoingia mjini
mtakutana na mwanamume akichukua mtungi wa maji; mfuateni mkaingine katika
nyumba atakayoingia yeye. Na mtamwambia mwenye nyumba, Mwalimu akuambia, Ki
wapi chumba wageni, nipate kula Pasaka humo pamoja na wanafunzi wangu? Naye
atawaonyesha chumba kikubwa orofani, kimekwisha andikwa; andaeni humo.
Wakaenda, wakaona kama walioambiwa, wakaiandaa pasaka. Hata saa ilipofika,
aliketi chakulani, yeye na wale mitume pamoja naye. Akawaambia, Nimetamani sana
kuila Pasaka hii Pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya
kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu. Akapokea kikombe,
akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambia ya
kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja.
Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ndio mwili wangu
unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Kikombe nacho
baada ya kula; akasema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu,
inayomwagika kwa ajili yenu,”
Usiku
wa Pasaka ulitolewa kwa Waisraeli miaka mingi sana kabla ya Kristo, lakini
ilionyesha kikamilifu usahihi wa mwezi na siku ambayo Kristo alipaswa kufa
msalabani. Ilionyesha kwamba yeye alipaswa kuwa ndiye Mwana Kondoo wa Mungu
asiye na dhambi wala waa lolote. Hii ni moja kati
ya sikukuu ambazo tumeamriwa kuzitunza na kuziadhimisha milele.
Siku nyingine muhimu zimeorodheshwa kawenye vitabu
vifuatavyo:
Kutoka 20:8 – 11
”Ikumbuke
siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini
siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako,
wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa
siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo,
akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa”
Lakini
Sabato ni lini? Sio Jumamosi kama wengine wanavyodhania. Pia sio Jumapili kama
wengine wanavyoadhimisha. Lakini katika mwaka huu imetokea tu kwamba inaangukia
siku ya Jumapili.Kwa mujibu wa mpango wa Mungu, mwezi wa kwanza unaanzia katika
mwezi wa Abibu. Mwezi huu wa Abibu unaandama kwenye kipindi kilicho karibu na
siku ambayo jua linapita katikati ya dunia kwenye mstari wa Ikweta, siku
inayolingana masaa ya usiku na mchana (mwanzoni mwa majira ya baridi). Kwa
mujibu wa utaratibu wa Mungu, huanza tarehe 18 Marchi, saa 12:00 jioni na huishia
Marchi 19 jioni. Siku saba baada ya Marchi 25 inakuwa ni siku ya saba ya au
Sabato. Hii hubadilika mwaka mmoja hadi mwingine kwa kuwa kalenda yetu haifuati
utaratibu wa Mwandamo wa Mwezi.
Mwanzo 1:14 ”Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la
mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili na majira na
siku na miaka;”
Warumi 14:5 - 6 ”Mtu
mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku; mwingine aona siku zote kuwa ni
sawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.Yeye
aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa
maana amshukuru Mungu; tena asiyekula,
hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu
No comments: