Latest News


More

TAMASHA LA PASAKA KUTIKISA DAR JUMAPILI HII

Posted by : Unknown on : Friday, April 18, 2014 0 comments
Unknown
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam wakati akielezea maadalizi ya Tamasha la Pasaka.
………………………………………………………………………………………………..
Tamasha la pasaka la Mwaka huu litakalozinduliwa rasmi April
20,jijini dar likibeba kaulimbiu ya “Tanzania kwanza haki huinua
Taifa”,litaemdendeshwa kwa namna ya Wadau wenyewe kuchagua waimbaji,aidha iwe
kutoka ndani ama nje ya nchi ikiwemo sambamba na mgeni rasmi.
Hayo yalibainishwa jijini Dar,mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mtendaji
wa Msama Promotions,ambao ndio wandaaji wa tamasha.Alifafanua kuwa wapenzi wa muziki huo
ndio watakaochagua waimbaji hao kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba 15327, kwa
kutumia mitandao yote ya simu.
“Tamasha la mwaka huu linakuja kwa mtindo wa kipekee
kabisa,ambapo wapenzi wa muziki wa injili watakuwa na fursa ya kuwachagua
wanamuziki watakao penda waje kutumbuiza ikiwemo na Mikoa litakapo fanyika tamasha
hilo, tofauti na miaka mingine na wale wote watakao pendekezwa tutawaleta kutoa
burudani”,alisema Msama.
Alisema,licha ya kuweka utaratibu huo,kumekuwa na changamoto
kubwa kwa wapenzi hao wa muziki wa injili ambao wanataka wanamuziki waliotoa
burudani wakati wa tamasha la krimasi akiwamo Solly Mahlangu kutoka nchini
Afrika Kusini.
Msama alisema,maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na
katika mazingira ya kwenda na wakati,limekuwa
na kauli mbiu ya “Tanzania kwanza haki huinua Taifa”.
Miongoni mwa waimbaji waliotikisa tamasha la Krismas
ambalo lilizinduliwa rasmi Desemba 25,mwaka jana jijini Dar,kabla ya
kuhamia mikoani,Ni Solly Mahlangu,Ephrahim Sekereti,Rose Muhando,Upendo
Kilahirio,Upendo Nkone,Edson Mwasabwite na wengineo,wakiwemo vijana wa Acapella
a.k.a The Voice.
2Msama akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari. 3Waandishi wa habari wakiwajibika

No comments:

Leave a Reply