Latest News


More

WAHITIMU WATIA FORA KWA UIMBAJI KANISA LA LIVING WATER CENTER - MAKUTI KAWE

Posted by : Unknown on : Monday, April 14, 2014 0 comments
Unknown
Saved under : ,
 Jana jumapili katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe yalifanyika mahafali ya wanafunzi wa kozi ya Life Transforming

Mahafali hayo ni ya kumi kufanyika na yalihudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo pamoja na ndugu jamaa na marafiki wa wahitimu hao na mgeni rasmi alikua Director wa kozi hiyo mwalimu Lilian Ndegi

Katika vikundi vilivyotia fora kwa uimbaji ni pamoja na kwaya ya wahitimu hao ambayo iliimba nyimbo mbili ambazo zilisababisha waumini kutokaa kwenye viti vyao na kusimama mara kwa mara na kuimba na kucheza pamoja na waimbaji hao
Pichani juu ni wahitimu hao wakiimba jukwaani
 Mgeni rasmi mwalimu Lilian Ndegi kulia akiwa ameketi pamoja na katibu wa kanisa la LWC - Makuti Kawe
Wahitimu hao wakiimba kwa furaha jana

Mgeni rasmi mwalimu Lilian Ndegi alishindwa kuvumilia na kujumuika na wahitimu kumtukuza Mungu.Hakika ilikua ni siku ya furaha kwa wahitimu hao

No comments:

Leave a Reply