Latest News


More

VYETI BANDIA VYA HIV VYAUZWA NCHINI UGANDA KAMA NJUGU

Posted by : Unknown on : Thursday, April 3, 2014 0 comments
Unknown
Saved under :

Idhaa ya BBC kitengo cha Afrika kimebaini kuna watu wanaonunua matokeo bandia ya vipimo vya virusi vya HIV yakionyesha hawana virusi hivyo nchini Uganda.
Picha za Filamu zilizonaswa kisiri zinaonyesha namna ilivyo rahisi kutoa hongo kwa wahudumu wa afya ili kupata vyeti hivyo bandia.
Baadhi ya watu wanaonunua vyeti hivyo visivyokubalika kisheria wanasema wamefanya hivyo ili kupata kazi, kusafiri kwenda ng'ambo ama kwa ajili ya kupata wapenzi wa ngono.
Mwandishi wa BBC wa Kampala Catherine Byaruhanga alilitembelea kliniki 15 bila ya kujitambulisha.
Kumi na mbili kati ya kiliniki hizo zilikuwa tayari kumpa vyeti bandia vya kuthibitisha kuwa hawana virusi vinavyosababisha ukimwi vya HIV.
Wanaosimamia kliniki hizo walitaka hongo kati ya Dola 10 na 20 kwa kila cheti.
Picha za video tulizopiga kisiri katika maduka ya kupiga chapa katika maeneo mengi ya mji mkuu wa Uganda, Kampala zinathibitisha kuwa mtu anaweza kuigiza cheti pia kwa urahisi sana.
BBC ilipomkabdihi Waziri wa Afya, Ruhakana Rugunda, ushahidi huo, alikubali kuwa hiyo ni changamoto kubwa lakini akasisitiza kuwa Serikali itafanya kila juhudi kuwakamata na kuwashitaki wanaohusika katika ufisadi huo.
Serikali ya Marekani hutoa kiwango kikubwa cha peza za miradi inayotumiwa kupambana na ukimwi nchini Uganda.
Balozi wa Marekani alitoa wito kwa viongozi wa taifa hilo kufanya bidii zaidi kupambana na kashfa hiyo.
Hata hivyo alisema kuwa hana uhakika kuwa Dola za Marekani hazijatumiwa katika kliniki hizo zinazotoa vyeti bandia.

No comments:

Leave a Reply