Leo katika kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Usharika wa Mwenge Umoja wa wanaume ambao leo umehudumu kwa mara ya kwanza katika Usharika huo umepata uongozi wao .
Umoja huo umeasisiwa takriban mwezi mmoja sasa na leo katika ibada zote mbili ibada imeongozwa na wanaume peke yao.Mara baada ya ibada hiyo wanaume hao walikutana na kuchagua viongozi watakaoongoza umoja wao hou.Kabla ya leo Umoja huo ulikua unaongozwa na kamati ya muda ambayo iliongozwa na mwenyekiti wa kamati ya mahusiano ya usharika huo mzee Tumaini Kichila na katibu wa muda bwana Allen Mushi
Pichani juu viongozi wa Umoja huo wakiwa katika picha ya pamoja pamoja na mwenyekiti wa kamati ya muda mzee Tumaini Kichila
Kutoka kushoto ni bwana Johanes Makundi (mweka hazina msaidizi), bwana Nathaniel Minja (mweka hazina, Mzee Tumaini Kichila (mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Umoja huo na mwenyekiti wa kamati ya mahusiano), bwana Allen Moshi (katibu msaidizi), Bwana Denis Ndyetabula (katibu), bwana Leonard Mushi (makamu mwenyekiti), na bwana Jonas Mbise (mwenyekiti)
Viongozi wa Umoja wa wanaume wa Usharika wa Mwenge wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kuchaguliwa jumapili ya leo
Mchungaji kiongozi wa Usharika wa Mwenge mchungaji Kaanasia Msangi akizungumza na uongozi mpya wa umoja wa wanaume wa Usharika huo mara baada ya kufanya uchaguzi wao jumapili ya leo.Waliosimama ni viongozi waliochaguliwa kuongoza umoja huo
No comments: