Written by Anonymous

HAPPY NEW YEAR 2015

by Anonymous / 06 Jan 2015

...

Written by Anonymous

MERY CHRISTMAS

by Anonymous / 25 Dec 2014

WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRISTMAS WE WISH U A MERY CHRIS...

Written by Anonymous

HAMUGEMBE PRAISE AND WORSHIP TEAM KUZINDUA ALBUM YAO MWEZI APRIL

by Anonymous / 31 Mar 2014

 Kikundi cha Hamugembe Praise and Worship Team cha mjini Bukoba  kinatarajia kuzindua album yao ya nyimbo za kusifu na kuabudu ...

Written by Anonymous

WE WISH YOU A HAPPY NEW YEAR 2014

by Anonymous / 31 Dec 2013

Leo ndio siku ya mwisho kwa mwaka huu 2013 na masaa machache yajayo tutaingia mwaka ujao 2014.Mtandao huu unawatakia kila la kheri na ba...

Written by Anonymous

KWAYA KUU YA USHARIKA WA AZANIA FRONT NDIO MABINGWA WA UIMBAJI WA K.K.K.T – DMP

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

Written by Anonymous

MASHINDANO YA UIMBAJI KWAYA KUU NGAZI YA DAYOSISI YA KANISA LA K.K.K.T (DMP) YAFANA USHARIKA WA MBEZI BEACH LEO

by Anonymous / 26 Oct 2013

Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...

KUTOKA MADHABAHUNI

IBADA KATIKA KANISA LA LIVING WATER CENTER MAKUTI KAWE JUMAPILI HII

Jumapili hii ilifanyoka ibada nzuri katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe ambapo kiongozi wa kanisa hilo Mtume Onesmo Ndegi  (pichani juu) aliongoza na kuhubiri Pichani juu Mtume Onesmo Ndegi akimtambulisha ndugu wa m...

More KUTOKA MADHABAHUNI
More NENO LA LEO
More MAHUBIRI
More MAOMBI

HABARI ZA KIDINI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI MHESHIMIWA MAKONDA AZINDUA VITABU VYA INJILI KANISA LA LIVING WATER CENTER KAWE KAWE

Mkuu wa wilaya ya Kinondoni mheshimiwa Paul Makonda jumapili hii alikua mgeni rasmi katika uzinduzi wa vitabu vya injili vya mwalimu Lilian Ndegi katika kanisa la Living Water Center - Makuti Kawe Bwana Makonda (pichani juu) alimsh...

More HABARI ZA KIDINI

More HABARI ZA KIDINI

JINSI YA KUMWEKEA KIJANA WAKO SHERIA

Posted by : Unknown on : Thursday, April 23, 2015 0 comments
Unknown
Saved under :




KIKWAZO

Kijana wako anasema wewe ni mkali sana. Hata hivyo, kwa sababu ya tamaa yako ya kiasili ya kumlinda unajiambia hivi, ‘Ikiwa nitalegeza sheria kijana wangu ataingia matatani!’
Unaweza kumwekea kijana wako sheria zenye usawaziko. Lakini kwanza unahitaji kujua ni nini kinachomfanya akasirishwe na sheria unazoweka.

KWA NINI HILI HUTUKIA

Dhana: Matineja wote huasi sheria; ni jambo lisiloepukika wakati wa ujana.
Jambo Hakika: Huenda tineja asiasi ikiwa wazazi wataweka sheria zenye usawaziko na kuzizungumzia pamoja naye.
Ingawa kuna mambo mengi yanayoweza kuchangia tineja kuasi, huenda wazazi bila kujua wakachochea jambo hilo ikiwa watashikilia sana sheria au wataweka sheria ambazo hazifai umri wa tineja. Fikiria mambo yafuatayo:
  • Kushikilia sana sheria. Wazazi wanapoweka sheria bila kuizungumzia pamoja na kijana wao, sheria hiyo inakuwa kama pingu inayombana badala ya kuwa mkanda wa usalama unaomlinda. Tokeo ni kwamba, huenda tineja akafanya kisiri mambo yaleyale ambayo wazazi wake wanamkataza.
  • Sheria ambazo hazifai umri wa tineja. “Kwa sababu nimesema,” jibu hilo linaweza kumridhisha mtoto mdogo, lakini vijana wanaobalehe wanahitaji maelezo zaidi—wanahitaji sababu. Isitoshe, hivi karibuni, kijana wako ataishi peke yake na atahitaji kujifanyia mwenyewe maamuzi muhimu. Kwa hiyo ni jambo linalofaa kwake ajifunze kufikiri vizuri na kufanya maamuzi mazuri sasa, wakati bado yupo chini ya uangalizi wako.
Lakini unaweza kufanya nini ikiwa inaonekana kwamba daima kijana wako hukasirishwa na sheria zako?

 MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA

Kwanza, tambua kwamba matineja wanahitaji—na hata wanataka sanakuwekewa mipaka. Kwa hiyo weka sheria, na uhakikishe kwamba kijana wako anazielewa. Kitabu Letting Go With Love and Confidence kinasema hivi, “Vijana wanaobalehe wanapowekewa mipaka iliyo wazi na kutazamia wazazi wawape mwongozo fulani, ni vigumu kwao kujiingiza katika tabia zisizofaa.” Kinyume cha hilo, wazazi ambao huhisi kwamba hakuna uhitaji wa kuweka sheria huwafanya vijana wao wafikiri kwamba wazazi wao hawajali. Na kwa hakika jambo hilo huwafanya waasi.—Kanuni ya Biblia: Methali 29:15.
Unawezaje kuonyesha usawaziko? Acha kijana wako aeleze anavyohisi kuhusu sheria za familia. Kwa mfano, ikiwa anaomba muda aliyowekewa wa kurudi nyumbani urekebishwe, msikilize anapoeleza sababu zake. Huenda ikawa rahisi zaidi kwa tineja kuheshimu na kufuata maamuzi unayofanya—hata kama hakubaliani nayo—ikiwa anahisi kwamba umemsikiliza kwa makini.— Kanuni ya Biblia: Yakobo 1:19.
Hata hivyo, kabla ya kufanya maamuzi kumbuka jambo hili: Matineja huwa na mwelekeo wa kutaka uhuru zaidi kuliko wanavyostahili, na wakati huohuo wazazi huenda wakawa na mwelekeo wa kuwapa matineja uhuru kidogo kuliko wanavyopaswa kuwapa. Kwa hiyo, fikiria kwa uzito ombi la kijana wako. Je, ameonyesha kuwa anaweza kutegemeka? Je, sheria inaweza kubadilishwa kwa sababu ya hali? Inapofaa, uwe tayari kubadilikana kulingana na hali.—Kanuni ya Biblia: Mwanzo 19:17-22.
Mbali na kusikiliza hisia za kijana wako, hakikisha pia yeye anajua mahangaiko yako kumhusu. Kwa kufanya hivyo, unamfundisha kutofikiria mapendezi yake tu bali pia afikirie hisia za wengine.—Kanuni ya Biblia: 1 Wakorintho 10:24.
Mwishowe, fanya uamuzi na ueleze sababu za uamuzi huo. Hata kama hapendezwi na uamuzi huo, yaelekea atafurahi kuwa na wazazi wanaomsikiliza na kutaka kujua maoni yake. Kumbuka, unamfundisha kijana wako anayebalehe kutenda kama mtu mzima. Kwa kumwekea kijana wako sheria zinazofaa na kuzizungumzia pamoja naye, utamsaidia awe mtu mzima mwenye kutegemeka.—Kanuni ya Biblia: Methali 22:6.

No comments:

Leave a Reply