Maswali
-
Unakasirika mara nyingi kadiri gani?
-
mara chache sana
-
pindi fulani
-
kila siku
-
-
Hasira yako ni kali kadiri gani?
-
kiasi
-
kali
-
kali sana
-
-
Ni nani ambaye mara nyingi hukukasirisha?
-
mzazi
-
mdogo wako
-
rafiki
-
Kwa nini ni muhimu
Unachoweza kufanya
-
Methali 29:22: “Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, na mtu yeyote mwenye mwelekeo wa ghadhabu ana makosa mengi.”“Ilikuwa vigumu sana kwangu kudhibiti hasira nilipokuwa tineja. Watu wa ukoo wa upande wa baba wana tatizo hilohilo. Sisi huuita udhaifu wa kuzaliwa. Ni vigumu sana kwetu kudhibiti hasira!”
—Kerri. Je, mimi ni mwenye hasira? Ikiwa ninakubali kuwa nimesitawisha sifa nzuri, je, inapatana na akili kutetea kwamba kushindwa kudhibiti hasira ni udhaifu wa kuzaliwa? -
Methali 15:1: “Jibu, linapokuwa la upole, hugeuza ghadhabu, lakini neno linaloumiza hufanya hasira ipande.”“Siri ni kujifunza kudhibiti hisia zako. Ukisitawisha sifa ya upole na kuzingatia sifa nzuri, kudhibiti hasira hakutakuwa tatizo tena.”
—Daryl. Kwa nini ni muhimu kuzingatia ninavyoitikia ninapochokozeka? -
Methali 26:20: “Pasipo na kuni moto huzimika.”“Kwa kawaida ninapoitikia kwa fadhili, hilo humtuliza mtu yule mwingine na tunaweza kuwasiliana kwa utulivu.”
—Jasmine. Maneno au matendo yangu yanawezaje kuongezea kuni kwenye moto? -
Methali 22:3: “Mtu mwerevu ni yule ambaye ameona msiba na kujificha, lakini wasio na uzoefu wameendelea mbele nao lazima waumie.”“Wakati mwingine ninahitaji tu kuondoka mahali hapo ili nipate muda wa kufikiria kilichotukia, kisha ninaweza kushughulika na jambo hilo baada ya kutulia.”
—Gary. Ni wakati gani unaofaa kuondoka mahali mlipo bila kumfanya mwenzako ahisi kana kwamba unampuuza? -
Yakobo 3:2: “Kwa maana sisi sote hujikwaa mara nyingi.”“Tunapaswa kujutia makosa yetu, hata hivyo, tunapaswa kujifunza kutokana nayo pia. Tunapaswa kuinuka tena tunapojikwaa na kuazimia kushughulikia hali vizuri zaidi wakati ujao.”
—Kerri.
No comments: