Latest News


More

Posted on : Saturday, September 5, 2015 [0] comments Label:

SEMINA YA MWALIMU MWAKASEGE KUFANYIKA VIWANJA VYA CHUO KIKUU JIJINI DAR ES SALAAM

by : Unknown
Semina ya Neno la Mungu Mjini Dar es salaam.

  Kuanzia tarehe 06 hadi 13 Septemba, 2015 tutakuwa na semina Dar es salaam uwanja wa Chuo Kikuu (UD) ,kila siku kuanzia saa 9 alasiri hadi 12 na mbili jioni. 

    Usikose kushiriki kusikiliza neno la Mungu na Mwl. Christopher Mwakasege, wagonjwa na wenye shida mbalimbali pia wataombewa. Utaweza kutazama live kwa kupitia Ustream pia
Posted on : Monday, August 17, 2015 [0] comments Label:

ASKOFU SHOO NDIYE MKUU WA KANISA LA K.K.K.T

by : Unknown
Askofu Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Frederick O. Shoo (kulia) akiwa na Askofu anayemaliza muda wake, Dk Alex Malasusa baada kuchaguliwa juzi usiku kwenye mkutano ulifanyika Arusha. Picha ya Mtandao 

Dar es Salaam. Askofu Dk Fredrick Shoo amechaguliwa kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), akichukua nafasi ya Dk Alex Malasusa aliyemaliza kipindi chake cha miaka minane.
Dk Shoo, ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, alichaguliwa juzi usiku katika siku ya tatu na ya mwisho ya mkutano mkuu wa 19 wa kanisa hilo uliofanyika Chuo Kikuu cha Tumaini (Tuma) jijini Arusha baada ya kuwashinda maaskofu wenzake wawili, katika uchaguzi uliokuwa na kila aina ya ushindani.
Waliokuwa wakichuana kuwania nafasi hiyo baada ya kupendekezwa na Halmashauri Kuu ya KKKT ni Askofu Dk Stephen Munga wa Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Askofu Charles Mjema wa Dayosisi ya Pare na Dk Shoo.
Mwenyekiti wa uchaguzi huo, Dk Malasusa, ambaye pia ni askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, alimtangaza Dk Shoo kuwa mkuu wa kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne baada ya kupata kura 153, huku Dk Munga akipata kura 67, ikiwa ni baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara tatu kutokana na mshindi kutopata zaidi ya theluthi mbili ya kura zote.
Kanuni za uchaguzi za KKKT zinaeleza kuwa mshindi atapatikana kwa kupata kura zisizopungua theluthi mbili ya kura zote zilizopigwa, iwapo mshindi hatapatikana katika duru la kwanza, majina mawili yaliyopata kura nyingi ndiyo yatakayopigiwa tena kura.
Iwapo theluthi mbili haitapatikana katika duru la pili, kura ya wingi au uchache itatumika kwa duru la tatu ili kumpata mshindi.
Katika kuhakikisha mshindi anapatikana, mkutano huo ulilazimika kutumia hatua ya wingi wa kura na Dk Shoo kuibuka mshindi.
Katika awamu ya kwanza, Askofu Mjema alipata kura 53, Dk Munga kura 81 na Dk Shoo kura 86, idadi ambayo haikufika theluthi mbili ya kura zote kulingana na kanuni za kanisa hilo jambo lililosababisha uchaguzi kurudiwa mara ya pili.
Dk Malasusa alitangaza matokeo ya awamu ya pili ya kura zilizopigwa ambapo Askofu Munga alipata kura 94 na Dk Shoo kura 124. Kura moja ikiharibika.
Kabla ya kuanza kwa mkutano huo wajumbe wa Halmashauri Kuu walipitisha majina matatu ya maaskofu waliowania nafasi hiyo na kuyapeleka kwenye mkutano huo ili yapigiwe kura.
Wajumbe wa mkutano huo mara baada ya kupewa karatasi za kupigia kura walikwenda katika vyumba maalum kwa ajili ya kumchagua askofu wanayemtaka, mara baada ya kuchagua walitakiwa kurejea ukumbini na kutumbukiza karatasi hizo katika vifaa vilivyoandaliwa kuhifadhia kura hizo.
Kauli ya Dk Shoo
Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Dk Shoo alimshukuru Mungu huku akionyesha mshangao wa kuchaguliwa kwake.
“Sijui nimepataje nafasi hii, ni nguvu ya Mungu tu kwa kweli. Kwa ushirikiano wa waumumini wote nitaweza kufanya kazi hii, naomba mniombee,” alisema.
Alichokisema Malasusa
Akizungumza katika ibada ya kufunga mkutano huo uliomalizika saa 6:00 usiku, Dk Malasusa alisema anamuachia madaraka Dk Shoo katika hali ya amani na utulivu, huku akiwapongeza viongozi na maaskofu wote wa kanisa hilo.
Awali kabla ya kuanza kwa uchaguzi huo, mkutano huo ulimchagua Alice Mtui wa Dayosisi ya Konde kuwa mwandishi wa kanisa hilo kwa kipindi cha miaka minne.
Alice alipigiwa kura 201 na wajumbe wa mkutano huo, huku kura za hapana zikiwa 17 na kura moja ikiharibika.
(Chanzo: Mwananchi Communications)


Posted on : Tuesday, July 21, 2015 [0] comments Label:

UNAWEZAJE KUSHUGHULIKA NA WAKWE ZAKO?

by : Unknown

Kushughulika na Wakwe

KIKWAZO

“Mke wangu aliwaambia wazazi wake tulipokuwa tukikabili matatizo. Kisha baba yake akanipigia simu ili kunishauri jinsi ya kushughulikia hali hiyo. Sikufurahia jambo hilo!”—James. *
“Mara nyingi mama mkwe husema, ‘Ninamkosa sana mwana wangu!’ Husema pia jinsi walivyokuwa karibu na mwana wake, jambo linalonifanya nihisi hatia kwamba nilifunga naye ndoa na kumletea mama yake maumivu ya moyo!”—Natasha.
Je, inawezekana kuzuia hali ya kushughulika na wakwe isiwe tatizo katika ndoa?

UNACHOPASWA KUJUA

Ndoa huanzisha familia mpya. Biblia inasema kwamba mwanamume anayefunga ndoa “atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake.” Mke pia anafanya hivyo kuelekea wazazi wake na mume wake. Anapofunga ndoa, Biblia inasema kwamba wawili hao wanakuwa “mwili mmoja.” Wanaanzisha familia mpya.—Mathayo 19:5.
Ndoa yako inachukua nafasi ya kwanza badala ya wazazi wako.Mshauri wa ndoa, John M. Gottman aliandika hivi: “Jukumu moja la msingi katika ndoa ni kwa mume na mke kuwa na umoja. Kuanzisha au kuchochea hisi hiyo ya kufanya mambo kwa umoja na mwenzi wako huenda kukatia ndani kutoshughulika sana na watu wa familia zenu.” *
Huenda ikawa vigumu kwa baadhi ya wazazi kuzoea badiliko hilo.Mume mmoja kijana anasema hivi: “Mara nyingi mke wangu alitanguliza kutimiza mahitaji ya wazazi wake kabla ya ndoa yetu. Baada ya kufunga ndoa, mama yake aliona kwamba nafasi yake imechukuliwa. Haikuwa rahisi kwake kukubali hilo.”
Huenda ikawa vigumu pia kwa baadhi ya wenzi wa ndoa wapya.James aliyenukuliwa mwanzoni anasema hivi: “Kuwa na wakwe si sawa na kuwa na marafiki unaochagua. Ni sawa na mtu fulani akuambie, ‘Umepata marafiki wawili wapya, iwe unapenda au la.’ Hata kama wanakuudhi bado ni sehemu ya familia yako!”

 UNACHOWEZA KUFANYA

Ikiwa wewe na mwenzi wako hamwelewani inapohusu jinsi ya kushughulika na wakwe, jitahidini kurekebisha tatizo hilo kwa pamoja. Fuateni ushauri huu wa Biblia: ‘Tafuteni amani, na kuifuatia.’—Zaburi 34:14.
Ili kufanya hivyo, fikiria hali zifuatazo. Kila hali inaonyesha mtazamo wa mume au mke. Hata hivyo, wote wawili wanakabili changamoto zilezile na kanuni zitakazoonyeshwa zinaweza kuwasaidia kushughulika na wakwe.
Mke wako anasema kwamba angefurahi ikiwa ungekuwa na uhusiano mzuri na mama yake. Lakini unaona ni vigumu kushughulika na mama yake.
Jaribu kufanya hivi: Zungumza na mke wako kuhusu tatizo hilo na uwe tayari kufanya marekebisho. Jambo kuu si namna unavyohisi kuhusu mama-mkwe bali jinsi unavyohisi kuhusu mwenzi wako uliyeapa kwamba utampenda. Wakati wa mazungumzo mwambie njia moja au mbili hususa utakazotumia kuboresha uhusiano wako na mama yake na ujitahidi kufanya hivyo. Kadiri anavyoona jitihada zako, mke wako atakuheshimu zaidi.—Kanuni ya Biblia: 1 Wakorintho 10:24.
Mume wako anasema kwamba unawahangaikia zaidi wazazi wako kuliko yeye.
Jaribu kufanya hivi: Zungumza na mume wako kuhusu tatizo hilo ili kujua maoni yake. Ni kweli kwamba mume wako hahitaji kuwa na hofu ya namna hiyo ikiwa unawaheshimu wazazi wako. (Methali 23:22) Hata hivyo, unahitaji kumhakikishia kupitia maneno na matendo yako kwamba bado unamthamini sana. Akiwa na uhakika huo, mume wako hatahisi kwamba anashindana na wazazi wako ili tu umthamini.—Kanuni ya Biblia: Waefeso 5:33.
Mke wako anaomba ushauri kwa wazazi wake badala ya kukuomba wewe.
Jaribu kufanya hivi: Zungumza na mke wako na mkubaliane kuhusu mambo ambayo mnaweza kuomba ushauri wa wazazi. Jitahidi kuwa mwenye kukubali sababu. Je, mara zote ni vibaya kuongea na mzazi kuhusu tatizo fulani? Ni wakati gani unaofaa wa kuzungumza nao? Mkikubaliana kuweka mipaka yenye usawaziko, hali hiyo haitakuwa tatizo. —Kanuni ya Biblia: Wafilipi 4:5.
by : Unknown
 Biblia inazungumzia juu ya vitu hivi tulivyonavyo ili tushinde maisha yetu ya dhambi:

(1) Roho Mtakatifu – kipawa kimojachapo ambacho Mungu ametupa (kanisa lake) kwa ajili ya kuwa na ushindi katika maisha ya kikristo ndani ya Roho Mtakatifu. Mungu anatofautisha mtendo ya mwili na matunda ya Roho Mtakatifu katika wagalatia 5:16-25. katika andiko hilo tunashauriwa kutembea katika uwepo wa Roho Mtakatifu. “waumini wote tayari wamejazwa na Roho Mtakatifu”,lakini hapa tunasisitizwa kupatia nafasi Roho Mtakatifu atutawale na kutuongoza. Hii ina maana ya kuwa tusikilize sauti yake tusije tukatenda mapenzi yetu wenyewe.

Tofauti ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuifanya maishani mwa mtu ni kama ile ya Petro, kabla hajajazwa Roho Mtakatifu alimkana Yesu mara tatu, na alikuwa mbeleni ameahidi kumfuata Yesu mpaka kwenye hatari ya kifo angekufa naye. Baada ya kujazwa na Roho alizungumza waziwazi na kwa ujasiri mbele ya wayahudi juu ya mwokozi katika siku ya pentekote.

Unatembea ndani ya Roho ukiwa humzuii anapotaka kujidhihirisha (“kumzima Roho” wathesalonike wa kwanza 5:19) na una kiu ya kujazwa naye kila wakati (Waefeso 5:18-21). Je mtu hujazwaje na Roho Mtakatifu? Kwanza ni kwa mapenzi ya Mungu kama vile ilivyo katika agano la kale. Alikuwa akichagua watu Fulani, kuwajaza kwa ajili ya kutekeleza kazi ama wadhifa Fulani (Mwanzo 41: 38; Kutoka 31:3; Hesabu 24:2; Samueli wa kwanza 10:10; na kadhalika.) Ninaamini kuwa kuna ushahidi katika Waefeso 5:18-21 na Wakolosai 3:16 yakuwa Mungu huchagua kujaza wale wanaojijaza Neno la Mungu kwa kuwa kote kote ni kujazwa uwezo wa Mungu.

(2) Neno la Mungu, Biblia – Timotheo wa pili 3:16-17 inasema ya kwamba Mungu ametupa neno lake ili lituandae katika kufanya kazi njema. Linatufundisha jinsi ya kuishi na cha kuamini, linatufunulia kama tumetenda makosa na kuturudisha katika njia ya sawa. Kama waebrania 4:12 inavyosema Neno la Mungu liko hai na lina nguvu ya kupenya ndani ya nafsi zetu kung’oa lile tatizo ambalo mwanadamu hangeweza kulitatua. Mwandishi wa zaburi azungumzia uwezo wa Neno la Mungu juu ya kubadilisha maisha ya watu katika zaburi 119:9,11,105 na aya nyengine. Joshua aliambiwa siri ya kushinda adui zake (inayoashiria pia vita vyetu vya kiroho) ni kwamba asilisahau Neno la Mungu bali alitafakari usiku na mchana ili akalitimize. Haya aliyatenda, ijapokuwa maagizo yenyewe hayakuwa na uhusiano na mambo ya kivita lakini yakampa ushindi katika vita vya kuimiliki nchi ya ahadi.

Hii ni sehemu ambayo mara nyingi tunaipuuza. Tunapenda kubeba biblia tukienda kanisani ama kusoma aya za kukariri lakini hatuyatilii maanani yale tuyasomayo. Hatuyatafutii nafasi maishani mwetu kiasi cha kutubu dhambi zetu na kumtukuza Mungu kwa kipawa hiki. Tunasoma tu kiasi cha kupata mtazamo Fulani juu ya wokovu lakini hatuongezi juhudi zozote katika kutafakari kwetu mara kwa mara kiasi cha kutufanya tuwe na afya nzuri kiroho.

Ni muhimu sana kwako ufanye tabia ya kusoma neno la Mungu. Kama bado hujazoea basi Roho anakusisitiza uwe na tabia ya kulisoma Neno la Mungu. Nina kushauri uwe na kumbukumbu ya yale uliyoyasoma kwa kuyanakili kwenye daftari lako au kwenye kompyuta. Biblia ndicho kifaa Roho hutumia katika maisha yetu na maisha yaw engine (Waefeso 6:17), ikiwa ni sehemu kubwa ya silaha mojawapo ambayo Mungu hutupa ili tupigane vita vya kiroho (Waefeso 6:12-18)!

(3) Maombi – Hii pia ni njia nyengine ambayo Mungu ametupatia. Njia hii wakristo wengi huitaja tu kwa maneno lakini hawaitumii. Tuna ibada za maombi na nyakati za maombi na kadhalika lakini hatuoni manufaa ya jambo hilo sawa na kanisa la kwanza (Matendo 3:1; 4:31; 6:4; 13:1-3, na kadhalika). Paulo mara kwa mara arudia kueleza vile alikuwa akiwaombea wale aliokuwa akiwahudumia. Lakini tunapokuwa peke yetu hatuitumii njiaa hii. Mungu ametuahidi mambo mazuri ya ajabu kuhusiana na maombi (Mathayo 7:7-11; Luka 18:1-8; Yohana 6:23-27; Yohana wa kwanza 5:14-15, na kadhalika.) Paulo analiongezea mkazo tena katika mafundisho yake juu ya kujiandaa kwa ajili ya vita vya kiroho (Waefeso 6:18)!

Je, ni muhimu kiasi gani njia hii? Tunapomtazama tena Petro, tunaona maneno ya kristo aliyomwambia kabla hajamkana kule Gethsemane. Yesu alipokuwa akiomba Petro alilala. Yesu akamwambia, “Kesheni mkiomba ili msiingie majaribuni: Roho inataka lakini mwili ni dhaifu” (Mathayo 26:41). Wewe pia kama Petro unataka kufanya mema lakini huna nguvu yakutosha kufanyia hayo. Lazima tufuate mausia ya Mungu, tuendelee kumtafuta, tukibisha na kumuuliza… na atatupatia nguvu ile tuitafutayo (Mathayo 7:7 na kuendelea). Lakini lazima tuitilie mkazo njia hii maishani mwetu ndiyo tufaulu. Sisemi ya kwamba maombi ndiyo njia maalum zaidi. La sivyo. Mungu ni wakutisha. Maombi ni kukubali hali zetu za udhaifu, ukuu wa Mungu mwenye nguvu na asiyeshindwa ili tupate uwezo huo huo tuweze kuyafanya yaliyo mapenzi yake (wala si yetu) (Yohana wa kwanza 5:14-15).

(4) Kanisa – Hii ni mojawapo ya njia tunazozifumbia jicho. Yesu alipowatuma wanafunzi wake aliwatuma wawili wawili (Mathayo 10:1). Tunaposoma juu ya habari za safari za wale wamishenari katika kitabu cha matendo ya mitume, hawakuenda mmoja mmoja bali katika makundi, wawili wawili au zaidi.Yesu alisema mahali wawili au watatu wamekusanyika kwa ajili ya jina langu, nami nitakuwa katikati yao (Mathayo 18:20). Anatuamuru tusiache kukusanyana pamoja kama kawaida za watu wengine zilivyo bali tuutumie wakati wa kuwa pamoja kwetu kwa kutiana moyo katika upendo na matendo mema (Waebrania 110:24-25). Anatuagiza kutubu dhambi zetu mmoja kwa mwingine (Yakobo 5:16). Katika habari za hekima katika agano la kale tunaambiwa ya kwamba chuma hunoa chuma mwenziwe, vivyo hivyo mtu huchangamsha sura ya rafiki yake (Methali 27:17) “kamba ya nyuzi tatu haikatiki rahisi.” “kuna nguvu katika umoja wa wengi (Mhubiri 4:11-12).

Baadhi ya watu ninaowafahamu wamepata kaka na dada katika kristo wanaotangamana pamoja au kwa simu na wanaelezana vile wanaendelea na maisha ndani ya kristo na wanawajibika katika kuombeana huku wakiishi maisha sawa na Neno la Mungu. Mabadiliko mara nyingine huja haraka na wakati mwengine polepole. Lakini Mungu ametuahidi ya kwamba kadri tunavyoendelea kutumia njia hizi alizotuwekea, ndivyo atatuletea mabadiliko maishani mwetu. Vumilia ukijua ya kuwa ni mwaminifu katika ahadi zake.
Posted on : [0] comments Label: ,

JEWEWE UNATOA FUNGU LA KUMI?

by : Unknown
Kutoa fungu la kumi ni jambo ambalo wakristo wengi hung’ang’ana nalo. Katika makanisa mengine kutoa fungu la kumi imesisitizwa kupita kiasi. Wakristo wengi pia hukataa kutii agizo la kutoa sadaka kwa Bwana. Kutoa fungu la kumi au sadaka inahitajika kuwa ni kitendo cha furaha na baraka. Lakini sivyo katika makanisa ya sasa.

Kutoa fungu la kumi ni agizo la agano la kale. Hili lilikuwa sharti la kila mwenye kupata zao au mfugo alete sehemu ya kumi ya pato hekaluni (mambo ya walawi 27:30; hesabu 18:26; kumbukumbu la torati 14;24; mambo ya nyakati ya pili 31:5). Wengine huchukulia ya kuwa fungu la kumi, katika agano la kale ilikuwa kama sehemu ya ushuru uliokuwa ukitolewa kwa ajili ya makuhani na walawi. Agano jipya haiamrishi wala kupendekeza mfumo halali wa kutolea fungu la kumi. Paulo asisitiza kuwa waumini watenge sehemu ya mapato yao kwa ajili ya kusimamia kanisa (wakorintho wa kwanza 16:1-2).

Agano jipya halielezi kiasi cha pato ambacho ni kitengwe kwa ajili ya kusimamia kanisa. (wakorintho wa kwanza 16:2). Kanisa la kikristo leo limechukua kile kiwango cha fungu la kumi kutoka kwa agano la kale na kukisisitiza kuwa ndicho kiwango cha chini cha mkristo kutoa. ijapokuwa agano jipya haitoi kiwango cha kutoa, inaelezea umuhimu na manufaa ya kutoa. Ni watoe sawa na uwezo wao “ kulengana na pato lake.” Wakati mwingine ina maana ya kutoa zaidi ya fungu la kumi, na mara nyingine kichache kuliko fungu la kumi. Yote hutegemea uwezo wa mkristo mwenyewe na mahitaji ya kanisa. Kila mkristo sharti aombe na kutafuta hekima kutoka kwa Mungu juu ya swala hili (Yakobo 1:5). “ kila mtu niatoe kile alicho azimia kutoa kutoka ndani ya moyo wake, si kwa manung’uniko wala kulazimishwa, kwa kuwa Mungu hupenda kwenye kutoa kwa moyo mkunjufu” (wakorintho wa pili 9:7).
Posted on : Thursday, May 21, 2015 [0] comments Label:

WALEMAVU WAFUNGA BARABARA YA KAWAWA NA UHURU JIJINI DAR LEO

by : Unknown
 KUNDI la walemavu, wajasiriamali na wafanyabiashara ndogo ndogo jana walifunga makutano ya barabara ya Kawawa na Uhuru (Karume) kwa muda wa saa tatu wakishinikiza Serikali iwapatie maeneo ya kufanyia biashara baada ya kuwaondoa katika eneo la Mtaa wa Kongo Kariakoo jijini Dar es Salaam. 
 Walemavu wakiwa wamekaa barabarani baada ya kufunga barabara hiyo leo jioni

 Walemavu wakiwa wanapiga soga katikati ya barabara leo

Umati wa wapita njia ukiangalia walemavu hao waliofunga barabara na kuleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara ya Kawawa na Uhuru

(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE (FS))
Posted on : [0] comments Label:

TUNAWEZAJE KUMKUMBUKA BWANA YESU KRISTO?

by : Unknown

Yesu Kristo—Tumkumbuke kwa Njia Gani?

Mwezi wa Desemba watu wengi ulimwenguni pote huona picha za Yesu akiwa mtoto. Akiwa amelazwa kwenye hori, yaani, sanduku kubwa linalotumiwa kulishia wanyama. Lakini je, tunapaswa kumkumbuka Yesu akiwa mtoto tu? * Acheni tuzungumzie njia muhimu zaidi ya kumkumbuka. Tunaweza kujifunza kutokana na jambo lililowapata wachungaji waliokuwa malishoni karibu na Bethlehemu usiku mmoja.
Ghafula malaika anawatokea wachungaji hao. Anawaambia hivi: “Mwokozi ambaye ni Kristo Bwana, amezaliwa kwenu.” Pia, malaika anawaambia watampata Yesu “akiwa amefungwa vitambaa na akiwa amelala katika hori.” Papo hapo, malaika wengine wengi wanatokea na kuanza ‘kumsifu Mungu.’
Ungehisije kama ungewasikia malaika wakimsifu Mungu?— Wachungaji wanafurahi sana! Wanasema: “Na twende moja kwa moja mpaka Bethlehemu tukaone jambo hili ambalo limetendeka.” Wanapofika huko wanamkuta “Maria na vilevile Yosefu, na yule mtoto mchanga akiwa amelala katika hori.”
Baadaye watu wengine wanakuja Bethlehemu ambako Maria na Yosefu wanakaa. Wachungaji wanapowaambia kuhusu kilichotukia, wote wanashangaa. Je, unafurahi kujua mambo hayo yenye kustaajabisha?— Watu wanaompenda Mungu wanafurahi kuyajua. Sasa acheni tuone ni kwa nini watu wanafurahi sana baada ya Yesu kuzaliwa. Ili tuelewe jambo hilo, tutachunguza mambo yaliyotukia kabla Maria hajaolewa.
Siku moja malaika anayeitwa Gabrieli anamtembelea Maria. Anamwahidi kwamba atazaa mtoto ambaye “atakuwa mkuu naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi.” Pia, Gabrieli anasema: “Atatawala akiwa  mfalme . . . na ufalme wake hautakuwa na mwisho.”
Maria anataka kujua hilo litawezekanaje kwa kuwa hajawahi kulala na mwanamume. Basi, Gabrieli anamfafanulia: “Nguvu za Aliye Juu Zaidi zitakufunika,” na “kile kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu.” Huo ungekuwa muujiza mkubwa! Kuuhamisha uhai wa Mwana wa Mungu kutoka mbinguni na kuuweka ndani ya tumbo la uzazi la Maria.
Je, umewahi kuona picha zinazoonyesha wanaume watatu wenye hekima pamoja na wachungaji wakimtembelea mtoto Yesu?— Ni jambo la kawaida kuona picha hizo wakati wa Krismasi. Lakini hazionyeshi jambo sahihi. Wanaume hao watatu walikuwa wanajimu, walizoea kufanya jambo ambalo Mungu alikataza. Acheni tuone kilichotukia walipofika. Biblia inasema: “Walipoingia ndani ya ile nyumbawakamwona huyo mtoto mchanga pamoja na Maria mama yake.” Wakati huo Yesu hakuwa mtoto aliyetoka tu kuzaliwa ndani ya hori; bali alikuwa akiishi pamoja na Yosefu na Maria katika nyumba!
Wanajimu walimpataje Yesu?— Ile “nyota” haikuwaongoza kwenda Bethlehemu kwanza, bali iliwaelekeza kwa Mfalme Herode huko Yerusalemu. Biblia inasema Herode alitaka kumpata Yesu ili amuue. Sasa fikiria jambo hili. Unafikiri ni nani aliyetumia kitu kilichofanana na nyota kuwaongoza wale wanajimu kwa Herode?— Si Yehova, Mungu wa kweli, bali ni mpinzani na adui yake, Shetani Ibilisi!
Leo, Shetani anawafanya watu wamfikirie Yesu kuwa mtoto aliyetoka tu kuzaliwa. Lakini Malaika Gabrieli alimwambia hivi Maria: “[Yesu] atatawala akiwa mfalme . . . , na ufalme wake hautakuwa na mwisho.” Sasa anatawala akiwa Mfalme huko mbinguni, na hivi karibuni atawaangamiza adui wote wa Mungu. Hilo ndilo jambo tunalopaswa kukumbuka kumhusu Yesu, na tunapaswa kuwaambia wengine kulihusu.
(Source:www.jw.org)