Latest News


More

Familia yahama nyumba kwa imani za ushirikina

Posted by : Unknown on : Monday, July 22, 2013 0 comments
Unknown
Saved under :


FAMILIA moja katika Kitongoji cha Matakani, Kata ya Bushiri, wilayani Pangani, imelazimika kuhama nyumba yao na kujihifadhi kwa majirani.
Hatua hiyo imetokana na nyumba hiyo kupigwa mawe juu ya bati usiku na mchana huku wanaopiga mawe hayo wakiwa hawaonekani.
Mmiliki wa nyumba hiyo, Boka Jack alisema tukio hilo ambalo analihusisha na nguvu za ushirikina, lilianza saa 6.01 usiku wa mkesha wa Mwaka Mpya.
Jack alisema ilianza kama mzaha usiku huo na walifikiri mawe hayo ni kwa ajili ya watu wanaosherehekea mwaka mpya kwa sababu kitongoji hicho hakina umeme na yeye anatumia umeme wa jua.
Alisema aliamua kutoa kioo juu ya paa usiku huo, lakini mawe hayo yaliendelea kupigwa hadi asubuhi.
“Mawe yanapigwa na yanadondoka chini mchana, sijui nifanyeje au ni huu umeme wa jua nilioweka kuna watu wananionea wivu,” alisema Boka.

Wakati mwandishi wa habari hizi akiwa kwenye mahojiano na Jack, mawe yalikuwa yakiendelea kupigwa juu ya bati huku milio ikisikika.
Kwa mujibu wa Boka, tangu siku hiyo wanalazimika kulala kwa majirani na kufunga duka lake, kwani kila anapojaribu kuingia ndani mawe yana zidi kupigwa hasa anapoingia dukani kuhudumia wateja.
Alisema tukio hilo analihusisha na imani za ushirikina na kuomba kama kuna mtu yeyote bila kujali imani, anaweza kumsaidia ampe msaada ili kuondokana na hali hiyo.

Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Athuman Mbilinyi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, haijawahi kutokea kijijini hapo.
Mbilinyi alisema licha ya jitihada za kuunda kikosi cha doria kuzunguka nyumba hiyo kuwatafuta wanaopiga mawe, mmoja alijaribu kupanda juu ya paa lakini alikoswa kupigwa jiwe la kichwa.

Alisema suala lililowashangaza hata mchana nyumba hiyo inapigwa mawe, hivyo kulazimika kuamini kwamba tukio hilo linahusiana na imani za ushirikina, ambazo zinalenga kuua maendeleo.

No comments:

Leave a Reply