Latest News


More

KUWEKA AKIBA NA KUWEKEZA KAMA MSINGI WA KUMTUMIKIA MUNGU – MWINJILISTI GODILIZEN MUSHI

Posted by : Unknown on : Sunday, October 20, 2013 0 comments
Unknown


Fursa inaendana na muda na wakati husika.Akihubiri katika ibada ya jumapili hii katika kanisa la K.K.K.T Usharika wa Mwenge Mwinjilisti wa kujitegemea Godilizen Mushi amesema swala la uchumi nalo lina majira na wakati wake

Amesema fursa pia hutoweka , muda wake unapoisha.Kila fursa ina misingi.Kama fursa uliyo nayo umejenga katika misingi mibovu kama ya udhalimu, utavuna udhalimu
Mungu hupenda kutumia vitu vichache ili kukupa vitu vingi zaidi
Kama huwekezi au kuweka akiba huwezi kumtumikia Mungu kwa uaminifu alisisitiza mwinjilisti Mushi
Mithali 6:6-11

Maneno haya yanatufundisha jinsi ya kuwekeza kama misingi ya kumtumikia Mungu
Zipo nyakati za neema na zisizo na neema
Wakati wa neema tunaweka akiba ya kutuwezesha kutumia wakati  usio  wa neema…Mithali 30:24 – 25
Alisema Chungu ni kiumbe mdogo sana na asie na nguvu lakina ana akili ya kuweka akiba
Tito 3:14

Alisema Displine ya mtu si kwa vitu vingi tu bali hata vile vilivyo vidogo.Usipokuwa na displine ya yale yaliyo madogo hata kwa makubwa huwezi kuwa na displine nayo

FAIDA ZA KUWEKA AKIBA
1.Kuepuka matumizi yasiyo ya lazima
2.Inakupa ujasiri wa yale uliyo nayo
3.Kama unataka kutawala ni lazima uwe na ardhi
Hata kanisa kama linataka liwe na nguvu wakati wowote ni lazima liwekeze katika ardhi
4.Akiba inapunguza msongo wa mawazo
5Mwinjilisti huyo alimalizia kwa kusema “SERVE FOR YOUR RETIREMENT:      Mhubiri 11:1-6

No comments:

Leave a Reply