Kwaya kuu ya Usharika wa Kinondoni ndio mabingwa wa uimbaji
wa jimbo la Kaskazini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya
Mashariki na Pwani
Akitangaza matokeo hayo Mchungaji mkuu wa jimbo na mchungaji
kiongozi wa Usharika waMbezi Beach mchungaji Anta Muro alisema kwaya kuu ya
Usharika wa Magomeni imeibuka washindi baada ya kupata alama 87.47
Wakitoa maoni yao kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo
majaji walioongoza mashindano hayo walisemavikundi vyote vimeimba kwa ustadi na
weledi mkubwa
Baadhi ya maoni waliotoa ambayo wamesema yanafaa kudumishwa
ni;
1.Kwaya zote zilivaa sare kama vilivyoambiwa na walipendeza
sana
2.Uimbaji mzuri na
utulivu ulizingatiwa
3.Waandishi wa muziki wa vikundi vyote walichapa miziki yao
4.Nyimbo za kiutamaduni zilikua za mtandao wa kitaifa
.Karibu kila upande wa Tanzania uliwakilishwa
5.Baadhi ya vikundi haswa chaguo la kwaya walitunga nyimbo
zao wenyewe.ali hiyo iendelee na sio kutegemea nyimbo za watu wengine
Mambo ambayo wanatakiwa wanakwaya na waalimu waboreshe
1.Note ziimbwe kwa thamani zake zisikatwe katwe
2.Vikubdi karibu vyote sauti ya kwanza ina nguvu sana.Hivyo
ziimbwe vizuri ili sauti nyingine nazi zisikike
3.Dynamics zifuatwe jinsi zilivyoandikwa .walimu awe mjanja
wa kuzifahamu nyimbo
4.Uandishi wa Note uzingatiwe utaalam wa maandishi
5.Matendo yanayofanyika jukwaani yawiane na ujumbe wa nyimbo
6.Matamshi ya maneno: Mfano Dunia usiseme Duni a matamshi yaendane na neon husika
7.Makondakta – alama za mwiho zisitumike na waalimu kama
hazipo kwenye note
8.Viongozi wanaoongoza (condactor) wawe chacu, kwani hii ni
sanaa, hivyo inabidi wawe wabunifu wa kutawala jukwaa
Mashindano hayo yaliratibiwa na majaji watatu wakiwepo mchungaji Kijalo , ndugu Gaitan na
ndugu Edwirn Andarson
Kiongozi wa kwaya ya Usharika wa Mbezi Beach ambao walichukua ushindi wa tatu akipokea kikombe kwa mkuu wa jimbo mchungaji Muro
Mwalimu kiongozi wa kwaya ya Usharika wa Kinondoni (Mwalimu Lwiza) ambao walichukua ushindi wa pili akipokea kikombe kwa mkuu wa jimbo mchungaji Muro
Kiongozi wa kwaya ya Usharika wa Magomeni ambao walichukua ushindi wa kwanza akipokea kikombe kwa mkuu wa jimbo mchungaji Muro.Mwalimu huyu ni ndugu na mwalimu wa kwaya ya Kinondoni
Kamisaa alikua mchungaji Mwaipopo
Washindi wa pili ni kwaya ya Usharika wa Kinondoni ambayo
imepata alama 87.22 na mshindi wa tatu ni kwaya ya Usharika wa Mbezi Beach
ambayo ilipata alama 87.08
Jumla ya kwaya 11 zilishindana na kwaya nyingine na alama
walizopata ni kama ifuatavyo;
Kwaya kuu ya Usharika wa Msasani alama 82.6
Kwaya kuu ya Usharika wa Manzese alama 79
Kwaya ya kuu Usharika wa Wazo Hill alama 81.97
Kwaya ya kuu usharika wa Sinza alama 82.38
Kwaya ya kuu Usharika wa Kunduchi Beach alama 81.95
Kwaya kuu ya Usharika
wa Bubju A alama 79.94
Kwaya kuu ya Usharika wa Kijitonyama alama 85.22
Kwaya kuu ya Usharika wa Ubungo alama 82.11
Kwaya ya Usharika wa Magomeni wakiimba kwenye mashindano hayo,
Kwaya hii inaongozwa na mwalimu Erick Lwiza
Washindi wa Pili kwaya kuu ya Usharika wa Kinondoni wakiimba kwenye mashindano hayo
Mwalimu wa kwaya hii ni mwalimu Kennedy Lwiza ambaye ni ndugu na mwalimu wa kwaya ya Usharika wa Magomeni ambao walichukua ushindi wa Kwanza
Hongera familia ya Lwiza kwa kumwimbia Mungu kwa ustadi
Kwaya kuu ya Usharika wa Mbezi beach ambao walichukua ushindi wa tatu
Mgeni rasmi mchungaji Muro ambaye pia ni mkuu wa jimbo la kaskazini akimpongeza kamisaa wa mashindano hayo mchungaji Mwaipopo kwa kazi nzuri walioifanya ya uamuzi
"Blog hii inawatakia kila la kheri wawakilishi hawa wa jimbo la kaskazini katika mashindano ya Dayosisi jumamosi ijayo huko kwenye usharika wa Mbezi Beach"
No comments: