Chama cha Kuweka na kukopa cha kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi ya Kaskazini, kimetumia zaidi ya shilingi 1.5 milioni kuwasaidia watu wasiojiweza na wanaoishi katika mazingira magumu
Hayo yalibainishwa jana na meneja wa chama hicho, Moniza Mlay baada ya kuwatembelea wazee wanaolelewa katika kambi ya kata ya Njiro Manispaa ya Moshi kwa lengo la kula nao chakula cha mchana
Chama kimekuwa kikitoa huduma mbalimbali kwa watu wasiojiweza na wale wanaoishi katika mazingira magumu wakiwemo wazee, alisema meneja huyo
Alisema kundi la wazee ni mojawapo ya makundi yaliosahaulika katika jamii na kwamba hali hiyo ndiyo iliyokisukuma chama hicho kuwasaidia kundi hilo na lile la watoto yatima
No comments: